Makala hii inahusu mada au mtu asiyejulikana sana. Kuna mashaka kama mada inastahili kuwa na makala katika kamusi. Onyo hili linaweza kuwekwa pia kama makala haionyeshi umaarufu, hata kama upo.

Watumiaji wanaombwa kushiriki katika majadiliano kama makala hii inafaa kubaki au la. Tazama:Wikipedia:Umaarufu

Unaweza kuondoa kigezo hiki kama majadiliano yametokea na washiriki walipatana.


Suleimani Ally Suleimani Kissamvu alizaliwa tarehe 13 Mei 1967 katika jiji la Dar es salaam , katika hospitali Ocean road.

ELIMU hariri

Suleimani Ally Suleimani Kissamvu, alipata elimu msingi katika Shule ya Msingi Zegero iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani tarafa ya Mzenga kuanzia mwaka 1976 hadi 1982, lakini hakubahatika kuendelea na masomo ya sekondari kupitia shule za serikali. Mwaka 1983 aliamua kujiunga na ami yake ambaye alikuwa kijishughulisha na shughuli za ufundi wa kushona nguo Vingunguti Dsm. Ambapo baada ya miaka mitatu alipata wazo la kujiendeleza zaidi kimasomo, mwaka 1986 alijiunga na Taasisi iliyojitambulisha kwa jina la "Dar polytechnical school" iliyokuwa inatoa masomo ya sekondari katika nyakati za jioni "Evening classes" ndani ya madarasa ya shule ya msingi Miburani iliyopo eneo la Sudani Temeke jijini Dar' salaam. Hata hivyo katika mwaka wa tatu, ulipofika mwaka 1988 alihama shule hiyo na kuhamia jirani, Shule ya Sekondari Mgulani Iliyo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) jirani kabisa na Uwanja wa Michezo wa Taifa.

Kwa bahati mbaya alishindwa kuendelea na masomo yake katika shule hiyo,Na hiyo ilitokana na mabadiliko ya ratiba za mahudhurio ya darasa katika shule yake mpya, kwa kuwa alitakiwa kufika shuleni saa 1 asubuhi na kutoka saa 8 mchana, hivyo kutokana na uchovu wa kwata kwa paredi za waalimu wenye nasaba za ki~jkt, hali ilikuwa si nzuri kabisa kwake, na ikapelekea kushindwa kufanya zile kazi alizokuwa azifanya akiwa nyumbani, kazi za ushonaji Na kwa kuwa ndizo kazi ambazo zilikuwa zinamuwezesha kwa maswarifu na kujikimu kwa mahitaji mengine, basi pia alishindwa kabisa kuendelea na masomo zaidi. Alibaki nyumbani na kuendelea na zile shughuli za ushonaji huku akiendelea kuangalia mazingira yatayomuwezesha kuendelea na elimu yake kwa wakati huo, hata hivyo hakufanikiwa. Kisamvu aliendelea kujibidiisha na shughuli zakevhizo za ushonaji ambapo kwa wakati huo sasa alishakuwa mkomavu katika kazi, na umri nao ulikuwa unazidi kuyoyoma, hivyo kutokana na msimamo wa itikadi ya kiimani, na umri haukumpa tena muda wa kuendelea kuishi peke

Maisha ya Ndoa hariri

Mwaka 1992 alifunga ndoa na bint wa kizaramo Bi Asha Athumani Mwinyitanga Buge ambaye chimbuko lake linapatkana Zaramo ya Mfuru, Kisarawe mkoani Pwani, na walibahatika kupata mtoto wa kike wa kwanza mwaka 2000 ambaye ni Zainabu Suleimani Ally S. Kissamvu na wa kiume aliezaliwa mwaka 2008 , Arishadi Suleimani Ally Kissamvu Hata hivyo mihemuko ya nguvu za ujana, mazonge ya kindoa pia uhuru wake katika dini, vilimpa ari, akiwa na mke huyo mmoja, pamwe na kabinti binti mmoja kwa wakati huo, ilipofika miaka minane baada ya kuzaliwa Zainabu, mwaka 2008 alifunga ndoa nyingine na bint mwingine wa kizaramo vilevile anayejulikana kwa jina la Kuluthumu Rajabu Chamkae, ambaye naye chimbuko lake linapatikana Masanganya, eneo ambalo nalo lipo Kisarawe mkoa wa Pwani. Mwenyezi Mungu amewaneemesha kupata watoto wawili wa kike, wa kwanza ni Arafa Suleimani Kissamvu aliyezaliwa mwaka 2009, na mwingine ni Amisa Suleimani Kissamvu alozaliwa tarehe 5/8/2014.


Chimbuchimbu yake hariri

Kama ilivyo kawaida ya binadamu wote nami nina asili na uzawa, baba yake Ally Suleimani Kissamvu ambaye kabla ya kuja hapa Dar' salaam alitokea Mzenga kijijini vilabwa mahala ambapo babu yeke Suleimani Kissamvu akiwa na wake zake wawili walifanya masikani yao, bi mkubwa Mwanafundi na bi mdogo Mwana Abdallah, Mwanafundi ndiye mama mzazi wa Mzee Ally S Kissamvu akiwa ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hiyo ya bibi na babu iliyokuwa na watoto sita, na ile ya bi mdogo na babu walilofanikiwa kupata watoto wawili. Vilabwa ni Kijiji Pia ambacho kipo wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani. Mama yake ni Mariamu Rashidi Mwimbe, ambaye alitokea kijiji cha jirani na hapo Vilabwa kiitwacho Zegero, mahala ambapo palikuwa ndipo makazi ya wazazi wake, Mzee Mwinyimadi Rashidi Mwimbe pamwe na bibi yao Bint Kondo wa Mirambo. Baba yao alipata kuishi na akina mama watatu katika nyakati tofauti kabla ya kifo chake, mama wa kwanza ndiye huyu Mariam Rashidi Mwimbe ambapo wakiwa pamoja alizaliwa dada yai mkubwa aitwaye Hadija Ally S Kissamvu, akifuatiwa na Suleyman Kisamvu na dada anaefuatia aliyefariki akiwa na umri wa miaka kumi na sita, yeye aliitwa Siwema Ally S Kissamvu. Baadae baba yake alioa mke mwingine ambaye ni Bi Mwanjaa Ally Faru, mama kutoka Kondoa katikati ya nchi ya Tanzania mkoani Dodoma ambapo wakiwa naye pia walibahatika kupata Mtoto mwingine wa kiume aitwae Hamisi Ally S Kissamvu ambae pia anajulikana kwa jina la Mkanyaji jr. Maisha yao ya ndo hayakudumu sana hatimaye Mzee alioa mke mwingine ambae waliishi naye hata umauti wake ulipomkuta mke huyo alijulikana kwa jina la Ashura bint Abdallah Mkungwa ambapo wakiwa na mama huyu pia walifanikiwa kupata mtoto wa kike aloitwa Sikudhani Ally S Kissamvu.

Safari Yake ya Ushairi hariri

Lakabu yake ya mwanzo alokuwa anaitumia kama mshairi ni "Mtulivu No1" jina ambalo limedumu kwa muda mrefu sana mwisho aliamua kulibadili na kujiita" Mzee wa Changamoto". Hadi sasa amefanikiwa kutoa kitabu kimoja cha mashairi kiitwacho KAMWAMBIE BABA

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Suleyman Kisamvu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.