Suni
Suni | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Dume la suni mashariki
(Neotragus moschatus) | ||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
| ||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||
Jenasi 2, spishi 3, nususpishi 4:
|
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Suni ni wanyamapori wadogo sana wa jenasi Neotragus na Nesotragus katika familia Bovidae. Wanyama hawa ni wadogo kabisa wa Bovidae (kimo sm 25–40 begani, urefu sm 40–60 na uzito kg 2.5–5.5). Wanatokea misitu minyevu na mikavu ya Afrika kusini kwa Sahara yenye kichaka kizito. Dume ana pembe fupi kwa urefu wa sm 3.5 hadi 13 kuhusiana spishi. Rangi yao ni kahawianyekundu lakini nyeupe upande wa chini. Suni hula majani, macho ya maua, machipukizi, nyoga, manyasi na mimea.
Zamani spishi zote ziliainishwa katika jenasi Neotragus lakini uchunguzi wa ADN ulifunua kwamba spishi hizi hazina nasaba kwa karibu. Suni mdogo labda ana nasaba na paa (Cephalophinae) huku spishi mbili nyingine zikiwa na nasaba na swala (Antilopinae).
Spishi
hariri- Neotragus pygmaeus, Suni Mdogo (Royal Antelope)
- Nesotragus batesi, Suni wa Bates (Bates's Pygmy Antelope)
- Nesotragus moschatus, Suni au Suni Mashariki (Suni)
- Nesotragus m. kirchenpaueri
- Nesotragus m. livingstonianus
- Nesotragus m. moschatus
- Nesotragus m. zuluensis
Picha
hariri-
Jike la suni mashariki
-
Jike la suni mdogo
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Suni kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.