Susan E. Cannon Allen

Mwanaharakati wa haki wa Kimarekani mwenye asili ya Afrika

Susan E. Cannon Allen (26 Mei 185912 Mei 1935) alikuwa mwanaharakati mwenye asili ya Afrika kutoka Illinois, Marekani. Alihudumu katika nyadhifa nyingi za utendaji katika vilabu kadhaa tofauti vya wanawake na alihusika katika kazi ya vilabu katika ngazi ya mtaa na jimbo.[1]

Susan E. Cannon Allen

Maisha binafsi na elimu

hariri

Cannon Allen alizaliwa huko Galesburg, Illinois, akiwa mtoto pekee wa James na Clarissa Richardson Cannon. Babu na bibi yake, Thomas na Susan Richardson, walikuja kaunti ya Knox kutoka Kentucky kupitia reli ya chini ya aridhi.[2]

Alihudhuria shule za Monmouth kwa lengo la kufundisha lugha za kigeni lakini hakuweza kutimiza hilo. Badala yake alifanya kazi ya umishonari katika Kanisa la United Presbyterian huko Galesburg, Illinois.[2]

Baadaye, mwaka 1877 aliolewa na John R. Allen ndoa ambayo ilidumu kwa miaka 56 hadi alipofariki mwaka wa 1933. Walikuwa na watoto ishirini pamoja, ni watoto nane tu kati yao walinusurika hadi utu uzima.[1][2]

Alifariki mnamo 12 Mei 1935, katika nyumba ya familia yake iliyopo 1412 Mulberry Street kufuatia ugonjwa wa mwaka mmoja.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 Davis, Elizabeth Lindsay (1922). The Story of the Illinois Federation of Colored Women's Clubs. Chicago, IL: University of Chicago. uk. 6–137.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Biographical Sketch of Susan Cannon Allen | Alexander Street, part of Clarivate". search.alexanderstreet.com. Iliwekwa mnamo 2023-12-19.
  3. Galesburg register mail “Death calls Susan Allen,” May 13th, 1935.
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Susan E. Cannon Allen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.