Wamarekani Weusi ni watu wanaoishi nchini Marekani wakiwa na mababu waliotoka Afrika.

Mwanamuziki Louis Armstrong
Mwanaharakati Martin Luther King
Mwanaanga Robert Curbeam

Mara nyingi mababu hao walipelekwa Marekani kama watumwa katika karne zilizopita.

Jina hili linaweza kutaja pia watu ambao wazazi wao au wenyewe walihamia Marekani hivi karibuni tu kutoka Afrika au kutoka nchi nyingine, hasa za Karibi na Amerika Kusini.

Watumwa walipelekwa Marekani kutoka Afrika kati ya miaka 1619 na 1807 hasa wakati usafirishaji wa watumwa kutoka Afrika ulipigwa marufuku.

Katika utamaduni wa Marekani kila mtu mwenye babu Mwafrika huhesabiwa kama "mtu mweusi" hata kama urithi wake wa kinasaba ni wa kichotara na sehemu kubwa ni wa Kizungu.

Utafiti kwamba kwa wastani, damu yenye asili ya Afrika imechangia 78.1%, ile ya Ulaya 18.5% na ya Kiindio 3%.

Siku hizi Wamarekani weusi wengi huishi mijini lakini bado kuna maeneo yenye Wamarekani weusi wengi mashambani kusini mwa nchi.

Kwa jumla kuna watu 39,151,870 wanaohesibwa kama Waamerika weusi na hao ni asilimia 13.5 ya Wamarekani wote. Wengi wao ni Wakristo Waprotestanti.

Mashuhuri kati ya Wamarekani weusi ni wanamuziki kama Louis Armstrong, wanasiasa kama Martin Luther King, Jr. au Barack Obama na waandishi kama Toni Morrison.

Marejeo