Ulinganifu

(Elekezwa kutoka Symmetry)

Ulinganifu (pia: mpachano[1], ing. symmetry ) ni tabia ya maumbo na magimba yenye sehemu zinazolingana. Kama sehemu za kitu ni kama pacha zinaitwa linganifu.

Tofauti kati ya umbo linganifu na silinganifu

Miili ya viumbehai wengi inafuata muundo wa ulinganifu kwa sababu macho, masikio, mikono, miguu na viungo vingine (si vyote!) viko mahali sawa upande wa kushoto kama upande wa kulia. Hii ni kama taswira geu inayoakisiwa. Mfuno huu unaweza kuitwa ulinganifu wa mstari[2] kwa sababu sehemu pacha ya geu inatokea kwenye mstari wa kioo au jira ya ulinganifu.

Kuna mfumo wa pili unaofuata nukta ya ulinganifu (pia: nukta ya pacha[3]). Hapo pande mbili zina umbali sawa na kitovu ambacho ni nukta ya ulinganifu.

Mifano ya maumbo linganifu hariri

Marejeo hariri

  1. "Ulinganifu" ni pendekezo la kamusi ya TUKI KKK/ESD, "mpachano" la KAST
  2. KAST inapendekeza "mstari pacha"; ing. linear symmetry
  3. KAST

Kujisomea hariri

Viungo ya Nje hariri

 
WikiMedia Commons