Tout Puissant Mazembe, maarufu kwa jina la TP Mazembe, ni klabu ya mpira wa miguu kutokea jiji la Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inayoshiriki ligi kuu ya nchini humo.[1]

TP Mazembe
Imeanzishwa11Feb 1935
UwanjaStade TP Mazembe
(Uwezo: 18,500)
MwenyekitiMoïse Katumbi Chapwe
MenejaLamine N'Diaye
LigiLinafoot
Tovutitovuti ya klabu

Historia

hariri

Tout Puissant Mazembe, ikiwa na thamani ya angalau milioni $10, ilianzishwa na watawa Wabenedikto waliokua wakisimamia shule ya Mtakatifu Boniface iliyopo Élisabethville (sasa Lubumbashi) katika jimbo la Katanga.[2] Mnamo mwaka 1939, wamisionari hao waliamua kuanzisha timu ya mpira wa miguu kwa ajili ya vijana wa shule waliokuwa wanashiriki skauti, mwanzoni, klabu hiyo ilipewa jina la Saint Georges FC, ikiwa ni njia ya kumuenzi kiongozi wa kikundi chao cha skauti. Klabu hiyo ilishiriki katika mashindano ya daraja la kwanza chini ya chama cha wachezaji wenyeji (FRASI) iliyoundwa na mfalme wa Ubelgiji. Ulipofika mwisho wa msimu, Georges walishika nafasi ya tatu.

Mnamo mwaka 1944, klabu hiyo ilianza kuonyesha mafanikio, na baadaye walibadilisha jina na kuitwa Saint Paul F.C., walipoamua kuchanganya wageni kwenye kuendesha timu, wamisionari waanzilishi waliamua kuachana na masuala ya usimamzi wa timu hiyo. Klabu ikaamua kubadili jina tena na kutumia jina la F.C. Englebertjina lililoakisi wazamini wakuu. Mwanzo wa jina la sasa"Tout Puissant" lilipatikana mwaka 1966, hii ni baada ya kushinda taji na kumaliza msimu huo bila kupoteza mchezo hata mmojawa.[1]

Mwaka 1960, Mazembe walibadilisha mfumo wa uongozi, hi ni mara baada ya DRC kupata uhuru mnamo 30 Juni 1960. Mwaka 1966, walishinda mataji matatu ya ndani, mataji hayo ni pamoja na National Championship, Coupe du Congo na Kombe la Katanga.

Miaka ya 1967 na 1968, walishinda mfululizo taji la African Cup of Champions. Walifanikiwa kufika hatua ya fainali mara nne mfululizo kuanzia mwaka 1967 mpaka 1970. Mazembe ndio timu ya kwanza Barani Afrika kushinda mfululizo taji la African Champions Cup. Mafanikio hayo yalikuja kujirudia kwa klabu ya Enyimba F.C mwaka 2003 na 2004.

Mazembe walipoteza ubora wao kwa takribani miaka 18. Shukrani ziende kwa Moïse Katumbi Chapwe gavana na mmiliki wa sasa wa klabu hiyo, kwani baada ya umiliki wake, Mazembe waliweza kuwa na kiwango bora cha ushindani katika soka la Afrika.

Mnamo Novemba 2009, Mazembe walifanikiwa kuchukua taji la Ligi ya vilabu bingwa Afrika. Walishinda dhidi ya Heartland F.C kwa kutoka sare ya 2–2, walishinda kwa ujumla wa magoli, sheria ya goli la ugenini.[3]

Kwa kushinda kwao taji hilo, Mazembe walifuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Vilabu duniani vya mwaka 2009 chini ya FIFA. Licha ya kuongoza kwa goli moja kipindi cha kwanza, walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Pohang Steelers kutoka Korea Kusini kwa kufungwa magoli 2–1.[4]. Mchezo uliofuata walipoteza kwa kufungwa 3–2 dhidi ya Auckland City FC. Walimaliza mashindano wakiwa nafasi ya 6.[5][6]

Mwaka 2010, walishinda taji la Klabu Bingwa Afrika kwa mara nyingine tena, Ilipofika Disemba, waliweza kuweka rekodi kwa kuwa klabu ya kwanza Afrika kufika hatua ya fainali kwenye mashindano ya Kombe la Vilabu duniani. Walifika hatua hiyo kwa kuzifunga timu za C.F. Pachuca ya Meksiko 1–0 hatua ya Robo Fainali na Sport Club ya Brazili 2–0 hatua ya nusu fainali.[7][8] Walipoteza hatua ya Fainali iliyochezwa Disemba 18 kwa kufungwa goli 3 – 0 dhidi ya Inter Milan ya Italia.[9]

TP Mazembe walishinda taji lao la tano la Klabu Bingwa Afrika mwaka 2015, Walishinda kwa matokeo ya Jumla 4 – 1 dhidi ya USM Alger kutoka nchini Algeria.[10]

Tanbihi

hariri
  1. 1.0 1.1 Bell, Jack. "TP Mazembe Surprises the World, Not Itself", Goal, 17 December 2010. (en) 
  2. Legge, David (17 Septemba 2009). "Win or bust for former champions Etoile". AFP. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Januari 2013. Iliwekwa mnamo 18 Septemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Mazembe clinch Champs Lge title". BBC Sport. 7 Novemba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Novemba 2009. Iliwekwa mnamo 3 Desemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "TP Mazembe 1 – 2 Pohang Steelers". ESPN. 11 Desemba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Juni 2011. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "TP Mazembe 2 – 3 Auckland City". ESPN Soccernet. 16 Desemba 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 24 Oktoba 2012. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "TP Mazembe continue journey". BBC Sport. 15 Desemba 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Desemba 2020. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. "TP Mazembe beat Pachuca at the Club World Cup". BBC Sport. 10 Desemba 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Desemba 2010. Iliwekwa mnamo 14 Desemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Inter stunned as Mazembe reach final". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Desemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "TP Mazembe 0 – 3 Internazionale". ESPN Soccernet. 18 Desemba 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Desemba 2010. Iliwekwa mnamo 18 Desemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "TP Mazembe beat USM Alger to win African Champions League". BBC Sport (kwa Kiingereza (Uingereza)). 8 Novemba 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 21 Machi 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu TP Mazembe kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.