Lubumbashi
Lubumbashi (zamani ilijulikana kwa Kifaransa kama Élisabethville na kwa Kiholanzi kama Elizabethstad) ni mji wa pili kwa ukubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (zamani ilijulikana kama Zaire) ukifuata mji mkuu wa taifa wa Kinshasa na ni kitovu cha biashara cha sehemu ya kusini ya nchi.
Lubumbashi L'shi - Lubum |
|||
| |||
Mahali pa mji wa Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo |
|||
Majiranukta: 11°40′0″S 27°29′0″E / 11.66667°S 27.48333°E | |||
Nchi | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo | ||
---|---|---|---|
Mikoa | Katanga Juu | ||
Serikali | |||
- Gavana | Moise Katumbi | ||
Eneo | |||
- Jumla | 747 km² | ||
Idadi ya wakazi (2015) | |||
- Wakazi kwa ujumla | 1,794,118 |
Mji huu ndio makao makuu ya Mkoa wa Katanga Juu ambao una madini ya shaba na uko karibu na mpaka wa Zambia. Makadirio ya idadi ya watu ni karibu milioni 1.8.
Jiografia
Lubumbashi uko karibu mita 1,000 juu ya usawa wa bahari. Mto Kafue unatiririka kando ya mpaka wa Zambia na uaendelea kupitia sehemu za Zambia hadi kuingia Mto Zambezi.
Historia
Wabelgiji walianzishwa mji wa Élisabethville (wakati mwingine Elizabethville katika Kifaransa, au Elisabethstad katika Kiholanzi) mwaka 1910. Mji huu ulifanikiwa na maendeleo ya kanda hii kwenye sekta ya madini ya shaba.
Wachimbaji migodi katika Élisabethville waligoma mnamo Desemba 1941 katika kupinga serikali ya Wabelgigi iliyowalazimisha kufanya kazi ngumu, kwa sababu ya "jitihada za vita".
Wabelgiji walianzisha Chuo Kikuu cha Élisabethville (sasa Chuo Kikuu cha Lubumbashi) mnamo 1954-1955. Katika uchaguzi wa manispaa wa Desemba 1957, watu wa Élisabethville waliwapiga kura wengi wa wagombea wa chama cha Nationalist Alliance de Bakongo, ambacho kilidai uhuru mara moja kutoka kwa Wabelgiji.
Élisabethville ulitumikia kama mji mkuu na kitovu cha biashara wa Jimbo la kujitenga la Katanga wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 1960-1963. Moise Tshombe alitangaza uhuru wa Katanga mnamo Julai 1960. Viongozi wa Kongo walimtia nguvuni akashtakiwa kwa uhaini Aprili 1961, hata hivyo alikubali kufutilia washauri wake wa kigeni na vikosi vya kijeshi kubadilishana na uhuru wake.
Tshombe alirejea Élisabethville lakini akakaidi mkataba akaanza kupigana upya. Vikosi vya jeshi vya Umoja wa Mataifa vilipinga wanajeshi wa Katanga na kuchukua udhibiti wa mji mnamo Desemba 1961 chini ya mamlaka makuu. Roger Trinquier, anayejulikana kwa machapishwo yake kuhusiana na vita, alikuwa mshauri wa kijeshi Kifaransa wa Rais Tshombe mpaka shinikizo la kimataifa, likiongozwa na Ubelgiji, lilisababishwa kuitwa tena na Ufaransa.
Mobutu Sese Seko hatimaye alipotwaa mamlaka alibadilisha jina la Élisabethville kuwa "Lubumbashi" na mwaka wa 1972 alibadilisha Katanga kuwa "Shaba."
Kongo aliingia uangamizaji mwingine wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990. Waasi wa Muungano wa Democratic Forces kwa Ukombozi wa Kongo waliteka Lubumbashi mwezi Aprili 1997. Kiongozi wa waasi Laurent-Désiré Kabila alizungumza kutoka Lubumbashi kujitangaza rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tarehe 17 Mei 1997 baada ya Mobutu Sese Seko kukimbia Kinshasa.
Wakati Laurent-Désiré Kabila aliamua kuteua bunge la mpito, mwaka 1999, uamuzi ulitolewa kufunya Bunge katika Lubumbashi, ili kuimarisha umoja tete wa nchi. Bunge liliwekwa katika jengo la Bunge la Wapinduzi wa Katanga, iliyokuwa na makao makuu yake katika jiji hili pia katika miaka ya 1960. Lubumbashi kwa hiyo ulikuwa mji wa mkuu wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia 1999 hadi 2003, wakati taasisi zote kuu za nchi zililetwa jijini Kinshasa.
Serikali
Kuanzia 2000-2006, Floribert Kaseba Makunko alikuwa meya wa Lubumbashi; baadaye alichaguliwa kwenye Bunge la Taifa mwaka 2006.
Utamaduni na uchumi
Mji huu una Chuo Kikuu cha Lubumbashi, ambacho kina maktaba. Kuna pia magazeti ya kila siku.
Lubumbashi unatumika kama kiungo muhimu cha kibiashara na viwanda vya kitaifa. Viwanda hivyo ni pamoja na viwanda vya nguo, bidhaa za chakula na vinywaji, ufiatuaji matofali, na uyeyushaji wa shaba.
Usafiri
Reli
Lubumbashi iko katika mstari wa reli baina ya Ilebo, Kindu, Sakania na Kolwezi; hata hivyo, kwa sababu ya ukosefu wa miundombinu ya uwekezaji katika mfumo wa reli, reli ina sifa ya kutoaminika.
Katika miaka ya 1960, sehemu ya kutoka kwa Mutshatsha hadi Lubumbashi iliwekewa umeme wa hadi 25 KV AC.
Angani
Lubumbashi ni nyumbani kwa uwanja wa ndege wa kisasa wa Lubumbashi International Airport. Kwa hiyo, mji huu unatumika kama kituo cha usambazaji wa madini kama vile shaba, kobalti, zinki, stani na makaa ya mawe.
Utalii
Vivutio katika mji huu ni pamoja na bustani, mbuga ya wanyama, Kiwanda cha Pombe na jumba la makumbusho la kanda la National Museum of Lubumbashi.
Marejeo
Kusoma zaidi
- Tim Butcher: Blood River - A Journey To Africa's Broken Heart , 2007. ISBN 0-7011-7981-3
Viungo vya nje
- "Villes de RD Congo - Lubumbashi" (kwa French). MONUC. 2006-05-29. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-17. Iliwekwa mnamo 2008-09-16.
{{cite web}}
: CS1 maint: unrecognized language (link) - Tuvuti isiyo rasmi ya Katanga
- Organization for street children in Lubumbashi
- Unofficial English language site Ilihifadhiwa 23 Aprili 2016 kwenye Wayback Machine.
- FallingRain Map - elevation = 177m (alama nyekundu ni reli)
11°40′S 27°28′E / 11.667°S 27.467°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Lubumbashi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |