Tarek Abdallah
Tarek Abdallah ni mwanamuziki wa Misri anaechezea kifaa cha muziki oud na mtunzi anayeishi Ufaransa.
Wasifu
haririTarek Abdallah alizaliwa huko Alexandria mwaka 1975.[1] Alikuwa amevutiwa na kifaa cha muziki oud tangu alipo kuwa mtoto, baada ya kumuona mchekeshaji akichezea ala hiyo kwenye TV, lakini kutokana na upinzani wa familia yake, ilimbidi asubiri hadi alipokuwa na umri wa miaka wa miaka kumi na tisa (19) ndipo aguse kwa mara ya kwanza katika maisha yake.[2] Akisoma na bwana Alexandria Hazem Shaheen, alikifanyia mazoezi kwa masaa 10 kwa siku ili aweze kuingia katika Nyumba ya Kiarabu ya Oud, shule ya oud iliyoundwa huko Cairo na bwana Iraqi Naseer Shamma.[2] Alihitimu kutoka hapo nakupata tuzo ya ubora. [1] Anaishi Marseille tangu mwaka 2001 na anafundisha musicology katika Chuo Kikuu cha Lumière Lyon 2. Anaelezea maendeleo ya mtindo wa muziki wa pambo na mbinu ya muziki wa ala. [1][2] Amealikwa katika nchi kadhaa za Kiarabu ili kutoa darasa la ustadi. [1] Alitoa albamu yake ya kwanza Wasla, akiwa na mpigaji ngoma Adel Shams El-Din, mwaka 2015.
Mtindo
haririAlbamu Wasla inatokana na muziki wa enzi ya Nahda kati ya mwaka 1910 na mwaka 1930. [3] [4] Inatokana na umbo la waslah, ambalo ni la muziki laini katika njia moja ya muziki yenye mdundo tofauti.[3]. Lakini kinyume na muziki wa enzi ya Nadha, muziki wake ni wa ala tu. [5] Baadhi ya midundo iliyotumiwa kwenye albamu hiyo ni migumu sana, mingine ilitumika mara moja tu kwenye mila, mingine iligunduliwa.[3] Kwa mujibu wa jarida la Kifaransa Les Inrockuptibles lilimsifu Abdalla kwa melodi za wazi na maadili yasiyolaumika.[4]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 "EGYPTE : TAREK ABDALLAH, Dans la grande tradition du ‘oud égyptien", Groupe Le Monde, 8 February 2015. Retrieved on 1 June 2016. Archived from the original on 2019-05-22.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 "A l’autre bout du casque - Tarek Abdallah et son disque Wasla", Radio France, 23 February 2015. Retrieved on 1 June 2016.
- ↑ 3.0 3.1 3.2 "Tarek Abdallah's Egyptian musical suites", Radio France, 1 February 2015. Retrieved on 1 June 2016.
- ↑ 4.0 4.1 "10 albums de musique du monde pour janvier", Les éditions indépendantes, 19 January 2015. Retrieved on 1 June 2016.
- ↑ "World Tarek Abdallah & Adel Shams El-Din", Groupe Le Monde, January 2015. Retrieved on 1 June 2016.