Tema ni mji wa bandari na viwanda nchini Ghana karibu na mji mkuu wa Accra kwenye mwambao wa Bahari ya Atlantiki. Mji wa Tema una wakazi 209,000 (2005).

Mahali pa Tema katika mkoa wa Accra, Ghana

Hadi mwaka 1961 Tema ilikuwa kijiji kidogo cha wavuvi. Tangu mwaka huo bandari kubwa ya Ghana ilijengwa Tema pamoja na viwanda vingi. Imekuwa kitovu cha viwanda nchini. Kuna mawasiliano kwa reli na barabara kuu kati ya Tema na Accra.