The Province ni gazeti la kila siku linalochapishwa na mtindo wa gazeti la porojo. Gazeti hili huchapishwa katika eneo la British Columbia na Kundi la Pacific Newspaper, kampuni shirika ya CanWest Global Communications. Limekuwa gazeti la kila siku tangu mwaka wa 1898.

The Province
Jina la gazeti The Province
Aina ya gazeti Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 1898
Nchi Kanada
Mhariri Wayne Moriarty
Mmiliki Shirika la CanWest Global Communications
Makao Makuu ya kampuni Vancouver, BC,
Nakala zinazosambazwa 167,746 - Desemba 2001
Tovuti http://www.theprovince.com

Kulingana na utafiti wa NADbank wa hivi majuzi, wasomaji wa The Province kila siku(kati ya Jumatatu na Ijumaa) ni 520,100 ,takwimu hii inalifanya kuwa gazeti linalosomwa sana katika eneo la British Columbia.Vilevile,usambazaji wa nakala katika siku sita ni nakala 167,746 kwa kila siku.

Historia hariri

Katika mwaka wa 1923, familia ya Southam ilinunua gazeti hili la The Province. Miaka ishirini na miwili baadaye katika mwaka wa 1945, wachapishaji wa nakala za jarida hili waligoma. The Province lilikuwa gazeti lililonunuliwa sana kati ya magazeti mengine yote jijini Vancouver likiwa mbele ya The Vancouver Sun na lile la News Herald. Kama matokeo ya mgomo huo wa wiki sita, gazeti hilo lilipoteza wanunuzi muhimu katika soko la magazeti ikifanya mauzo yao yapungue. Gazeti hili lilishuka hadi nafasi ya tatu katika mauzo ya magazeti. Katika mwaka wa 1957, magazeti ya The Province na The Vancouver Sun yaliuzwa kwa kampuni ya Pacific Press ambayo ikamilikiwa na kampuni zote mbili (Vancouver Sun na The Province).

Stesheni za redio za CFCB / CKCD hariri

Mnamo 23 Machi 1922, The Province lilianzisha stesheni ya redio ya CFCB iliyotangaza habari mbalimbali na ripoti za soko la hisa. Kulikuwa na muhtasari za habari siku nzima zikifuatiwa na muziki. Stesheni hii ,kwa kawaida, ilikuwa ikifungwa saa nne ya usiku. Stesheni hii ilibadilisha jina lake kuwa CKCD katika mwaka wa 1923, na ikahamia mfumo wa usambazaji wa 730kHz katika mwaka wa 1925. Usimamizi wa gazeti hilo, The Province , likachukuliwa na kampuni ya Pacific Broadcasting katika mwaka wa 1933 huku The Province likiendelea kuipa stesheni hiyo ripoti na habari mbalimbali za kutangazwa.

Katika mwaka wa 1936, shirika jipya lililokuwa limeundwa la Canadian Broadcasting Corporation(liliundwa ili liwe shirika la utangazaji na pia la kusimamia sheria za utangazaji - jukumu hili la pili,hapo awali, lilikuwa la Idara ya Umarina na Uvuvi) liliagiza CKCD kurudisha kibali chake na kufunga kazi yake yote. Stesheni ya CKCD ilitangaza habari yake ya mwisho katika mwezi wa Februari 1940. [1]

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri