The Tech (gazeti)
The Tech, lililochapishwa kwa mara ya kwanza 16 Novemba 1881, ni gazeti kongwe kabisa na kubwa kabisa la kampasi katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (Massachusetts Institute of Technology-MIT). Linapatikana katika eneo la Cambridge, Massachusetts. Matoleo huchapishwa Jumanne na Ijumaa katika mwaka wa masomo, kila siku katika kipindi cha wanafunzi wapya kuripoti, mara moja kwa wiki katika mwezi wa Januari na mara kadhaa katika majira ya joto. Nakala huchapishwa na husambazwa kote katika kampasi ya MIT katika asubuhi hiyo ya uchapishaji.
The Tech | |
---|---|
Jina la gazeti | The Tech |
Aina ya gazeti | Gazeti la Wanafunzi wa Chuo Kikuu |
Lilianzishwa | 16 Novemba 1881 Kwenye mtandao : 1993 |
Eneo la kuchapishwa | Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts Maarufu kama: MIT |
Nchi | |
Mwanzilishi | Arthur W. Walker |
Mchapishaji | Charles River Publishing (2000-2009) Saltus Press |
Makao Makuu ya kampuni | Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts |
Tovuti | http://tech.mit.edu/ |
The Tech ndilo gazeti la kwanza kuchapishwa kwenye mtandao wa tarakilishi za ulimwengu. Katika ukurasa mmoja wa tovuti yake kumeandikwa "Gazeti la kwanza la dunia kwenye mtandao ,lilianzishwa mwaka wa 1993." Hapo awali, StarText , mfumo wa aina ya videotex ya Fort Worth Star- Telegrams wa kuonyesha makala ya magazeti kwenye skrini za kompyuta, ilianzishwa katika mwaka wa 1982 katika Fort Worth, Texas. Ingawaje, mfumo wa StarText haukutumika kwenye mtandao mpaka mwaka wa 1996.Katika mwaka wa 1987, gazeti la Middlesex News (Framingham, Massachusetts) ilianzisha Fred Kompyuta, mfumo wa BBS uliotumika kuangalia toleo la siku inayofuata na ,hapo baadaye, mfumo huu ulitumika kuandaa makala ya filamu ya gazeti hili.
Karibu kila toleo la Tech hupatikana kwenye tovuti na matoleo mengi hupatikana kama faili za PDF. Kwa mfano, toleo la kwanza lililochapishwa: The Tech (16 Novemba 1881).[1] Lilihaririwa na Arthur W. Walker, kisha likachapishwa na Alfred Mudge & Son, Printers, wanaopatikana katika barabara ya 34 School Street katika Boston. Hivi sasa, gazeti la Tech linachapishwa na kampuni ya uchapishaji Mass Web Printing Company, kitengo cha Kundi la Phoenix Media/Communications Group linalochapisha Boston Phoenix. Kutoka mwaka wa 2000 - 2009, Tech lilichapishwa na Charles River Publishing katika Charlestown na ,kwa muda mfupi, Saltus Press katika Worcester, baada ya Saltus kununua CRP.
Kumbukumbu za The Tech zinapatikana katika tovuti yao.[2]
Wanafunzi mashuhuri
hariri- Karen W. Arenson - Mwandishi wa Elimu wa The New York Times.
- O. Reid Ashe, Jr - Afisa Mkuu wa Operesheni wa Media General.
- Simson Yale Garfinkel - Mwandishi wa Technology Review, Wired na Boston Globe.
- Arthur Hu - Mwandishi wa Asian Week. Makala yake yalizungumza kuhusu idadi inayoongezeka ya wanafunzi Wamerika wa asili ya Kiasia katika miaka ya 1980 na makala yake yalinukuliwa na Thomas Sowell.
- Tom Huang - Mhariri Msaidizi wa The Dallas Morning News.
- Karen Kaplan - Mwandishi wa Kisayansi wa Los Angeles Times.
- James R. Killian, Jr - Rais wa 10 wa MIT.
- Norman D. Sandler - mwandishi mshirikishi wa White House wa United Press International.
- Larry Stark (jina lake la uandishi lilikuwa Charles Foster Ford) - mkosoaji wa maigizo aliyejulikana sana wa Boston.Stark alianza kuandika makala ya The Tech katika miaka ya 1962 - 1964. Makala ya Stark kuhusu maigizo ya Arthur Kopit, Oh Dad, Poor Dad, Momma's Hung You in the Closet na I'm Feeling So Sad yanapatikana katika tovuti ya The Tech [3]
- Keith J. Winstein - Mwandishi wa habari kwa gazeti la The Wall Street Journal.
Viungo vya nje
hariri- The Tech Tovuti rasmi Ilihifadhiwa 14 Januari 2010 kwenye Wayback Machine.