Thomas Alva Edison (11 Februari 1847 - 18 Oktoba 1931) alikuwa mvumbuzi mashuhuri na mfanyabiashara nchini Marekani. Aliboresha vifaa kama balbu ya umeme, mikrofoni na kugundua gramafoni. Utafiti na uvumbuzi wake ulihusu hasa mitambo ya umeme. Akajishughulisha pia na mtandao wa ugawaji wa umeme.

Thomas A. Edison
(Kiingereza) A Day with Thomas Edison (1922)
Phonograph ya Edison ilikuwa machine ya kwanza iliyotunza sauti

Edison alizaliwa katika familia ya Ohio kama mtoto wa saba akasoma miezi michache tu shuleni alipofukuzwa kwa sababu hakupenda kutulia na kusikiliza akafundishwa na mamake nyumbani. Aligonjeka mara kadhaa na tokeo moja ilikuwa ya kwamba kuanzia umri wa miaka 15 alikuwa karibu kiziwi.

Alipata kazi yake ya kwanza kwenye kampuni ya telegrafu. Kazi hii ilimwachia nafasi ya kujisomea na kutengeneza vifaa vyake vya kwanza. Alipokuwa na umri wa miaka 21 alitengeneza machine ya kuhesabu na kukadiria kura kwenye chaguzi.

Mwaka 1877 alibuni mashine ya kushika sauti ikaitwa "phonograph" na kuwa mashine mama wa gramofoni.

Akaendelea kuboresha balbu ambayo hakuvumbua lakini hadi kwake balbu zilidumu muda mdogo tu; mwaka 1879 alifaulu kutengeneza balbu iliyotoa mwanga masaa 40 na baada ya miaka mitatu ya kuboresha balbu hii tena alifikia kwa masaa 1,000.

Edison alivumbua mengi; mapato kutokana na mauzo ya mitambo yeke yalimruhusu kujenga maabara makubwa na kuwaajiri muhandisi na wasidizi wengi.

Alitambua mapema ya kwamba kufaulu kwa mitambo ya umeme kulihitaji mtandao wa usambazaji wa umeme. Aliendelea kutengeneza swichi na mita ya kuhesabu matumizi ya umeme.

Tangu mwaka 1881 kampuni ya Edison ilianza kuweka waya za umeme mjini New York na 1882 alimaliza kituo cha umeme cha kwanza. Hadi 1911 kampuni yake ilkuwa na vituo 33 vilivyotoa umeme kwa balbu milioni 4.6 na wateja 108,500.

Kampuni yake iliendelea kuwa kampuni kubwa ya General Electric.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: