Thug Life: Volume 1
Thug Life: Volume 1 ilikuwa albamu ya kwanza kutolewa na kundi la Thug Life, lililoanzishwa na rapa Tupac Shakur, na ilitolewa mnamo tar. 26 Septemba 1994. Awali albamu ilitolewa na studio ya Shakur ya Out Da Gutta Records. Kwa kufuatia upondaji mkubwa juu ya muziki wa gangsta rap kwa kipindi hicho, toleo halisi la albamu likatiwa kapuni na kurekodiwa upya na nyimbo nyingine mpya kibao na zile baadhi za awali kukatwa. Ilisemekana kwamba 2Pac alitengeneza matoleo mengine mawili ya albamu hii, yenye nyimbo kibao ambazo bado hazikutolewa. Kundi linaunganishwa na Big Syke, Macadoshis, Mopreme, The Rated R na Tupac Shakur. Miongoni mwa nyimbo kali kutoka kwenye albamu hii ni pamoja na "Bury Me a G","Cradle to the Grave", "Pour Out a Little Liquor", "How Long Will They Mourn Me?" na "Str8 Ballin". Mnamo mwaka wa 1996 Big Syke na Shakur walipanga watengeneze toleo la pili la Thug Life: Vol. 2 - Out On Bail ambayo ilitakiwa itolewe na studio ya Makaveli Records, lakini yale mauaji ya mwisho ya mjini Las Vegas yamesababisha hili lisiwe kweli[1]. Japokuwa awali albamu ilitolewa chini ya studio ya Shakur ya Out Da Gutta, Amaru Entertainment, studio ambayo inamilikiwa na mama yake Tupac Shakur, imekuwa ikipata haki zake. Thug Life: Volume 1 ilitunukiwa Dhahabu[2]
Thug Life: Volume 1 | |||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Studio album ya Tupac na Thug Life | |||||||||||
Imetolewa | 26 Septemba 1994 | ||||||||||
Imerekodiwa | 1993-1994 | ||||||||||
Aina | G-Funk, West Coast hip hop | ||||||||||
Urefu | 42:28 | ||||||||||
Lebo | Interscope/Atlantic Records (First pressing) Amaru/BMG/Jive Records (Second pressing) |
||||||||||
Mtayarishaji | Nate Dogg, Easy Mo Bee, Warren G, Johnny "J", Mopreme, Syke | ||||||||||
Tahakiki za kitaalamu | |||||||||||
Wendo wa albamu za Tupac na Thug Life | |||||||||||
|
Orodha ya Nyimbo
hariri# | Jina | Mwimbaji | Mtayarishaji |
---|---|---|---|
1 | "Bury Me a G" | 2Pac, Mopreme, Rated R, Big
Syke, Macadoshis, Natasha Walker na Stretch |
Thug Music |
2 | "Don't Get It Twisted" | Mopreme, Macadoshis na Rated R | Jay na Mopreme |
3 | "Shit Don't Stop" | 2Pac, Macadoshis, Rated R,
Mopreme, Big Syke na Y.N.V. |
Thug Music |
4 | "Pour Out a Little Liquor" | 2Pac | Johnny "J" |
5 | "Stay True" | 2Pac, Stretch na Mopreme | Thug Music |
6 | "How Long Will They Mourn Me?" | 2Pac, Nate Dogg, Big
Syke, Rated R na Macadoshis |
Nate Dogg na Warren G |
7 | "Under Pressure" | 2Pac na Stretch | Thug Music |
8 | "Street Fame" | 2Pac, Mopreme, Big Syke na Rated R | Stretch |
9 | "Cradle to the Grave" | 2Pac, Mopreme, Rated R,
Macadoshis na Big Syke |
Jay Choi na Big Syke |
10 | "Str8 Ballin" | 2Pac | Easy Mo Bee |
Nafasi ya Chati ya Albamu
haririMwaka | Albamu | Nafasi za Chati | |
Billboard 200 | Top Hip Hop Albums | ||
1994 | Thug Life Vol. 1 | #42 | #6 |
Nafasi za Chati za Single
haririMwaka | Wimbo | Nafasi ya Chati | |||
The Billboard Hot 100 | Hot R&B/Hip-Hop Singles & Tracks | Hot Rap Singles | |||
1995 | "Cradle to the Grave" | - | #91 | #25 |
Marejeo
hariri- ↑ http://www.donkilluminati.com/interviews.htm Ilihifadhiwa 17 Mei 2010 kwenye Wayback Machine. Exclusive Big Syke Interview
- ↑ [1] Ilihifadhiwa 4 Septemba 2015 kwenye Wayback Machine.Riaa Searchable Database Thug Life
Viungo vya nje
hariri
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thug Life: Volume 1 kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |