Tiasa Adhya

Mhifadhi kutoka India (Uhindi)

Tiasa Adhya (alizaliwa mnamo 1987) ni mhifadhi na mwanabiolojia wa wanyamapori kutoka India.[1] Hufuatilia paka wavuvi na amepokea tuzo ya Nari Shakti Puraskar.

Tiasa Adhya alisomea zoolojia katika Chuo Kikuu cha Calcutta na alifanya utafiti katika chuo kikuu (University of Trans-Disciplinary Health Sciences and Technology (TDU)).[1] Adhya anafanya kazi katika Umoja wa Kimataifa wa Uhifadhi wa Mazingira (IUCN). Kama sehemu ya Tume ya Kuishi kwa Spishi, hufuatilia paka wavuvi huko Bengal Mashariki.[2] Pia alishiriki kuanzisha Mradi wa Paka wa Uvuvi.[3]

Adhya amepokea tuzo ya Nari Shakti Puraskar na ya 2022 Future For Nature kwa kutambua mafanikio yake.[1][4]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tiasa Adhya kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.