Tiberia (pia: Tiberias; awali: Yam Ha-Kineret) ni mji wa Israeli kwenye pwani ya ziwa Galilaya, ambalo pengine linaitwa ziwa au bahari ya Tiberia (Yoh 6:1).

Bandari ya Tiberia.

Mji huo ni maarufu kwa sababu Injili zinautaja kuhusiana na Yesu kuzidisha mikate na samaki kwa ajili ya umati (Yoh 6:23) na baada ya ufufuko wake kuwaandalia wanafunzi wake mikate na samaki juu ya makaa (Yoh 21:1).

Mwaka 2019 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa 44,779 [1].

Marejeo

hariri
  1. "Population in the Localities 2019" (XLS). Israel Central Bureau of Statistics. Retrieved 16 August 2020.