Ufufuko wa Yesu
Ufufuko wa Yesu ndio tukio kuu lililotangazwa daima na Kanisa lake lote kuhusu mwanzilishi wake, Yesu Kristo, kuanzia ushuhuda wa Mitume wa Yesu na maandiko ya Agano Jipya, hususan Injili, hadi leo.
Kadiri ya imani hiyo, siku ya tatu baada ya kuuawa msalabani Ijumaa kuu, Yesu alifufuka mtukufu akiacha kaburi lake na vitambaa vyote vilivyotumika kumzikia.
Tangu Jumapili hiyo na kwa muda wa siku arubaini (kadiri ya Matendo ya Mitume 1:3), yeye aliendelea kuwatokea mara kadhaa wanafunzi wake, hadi alipoonekana nao akipaa mbinguni huku akiwabariki.
Tukio hilo linaadhimishwa kila mwaka kwenye Pasaka ya Kikristo na kila wiki kwenye Dominika.
Kwa Wakristo, ufufuko wa Yesu ndiyo sababu na kielelezo cha ufufuko wa waadilifu wote siku ya kiyama.
Mahali na tarehe
haririKadiri ya Injili, kaburi la Yesu lilikuwa karibu na Golgotha-Kalivari, nje kidogo ya ngome ya Yerusalemu.
Injili hazitaji tarehe wala mwaka wa tukio hilo. Wataalamu wengi, kwa kulinganisha habari zake na za vyanzo vingine vya historia ya Dola la Roma na vya dini ya Uyahudi, wanakadiria siku hiyo kuwa tarehe 9 Aprili mwaka 30.
Habari katika Injili ya Marko
hariri16:1 Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. 2 Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza; 3 wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakayetuvingirishia lile jiwe mlangoni pa kaburi? 4 Hata walipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno.
5 Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. 6 Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka. 7 Lakini enendeni zenu, mkawaambie wanafunzi wake, na Petro, ya kwamba awatangulia kwenda Galilaya; huko mtamwona, kama alivyowaambia. 8Wakatoka nje, wakakimbia kutoka kaburini; kwa maana wameingia tetemeko na ushangao; wala hawakumwambia mtu neno, maana waliogopa.
9 Naye alipofufuka alfajiri siku ya kwanza ya juma, alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambaye kwamba alimtoa pepo saba. 10 Huyo akashika njia akawapasha habari wale waliokuwa pamoja naye, nao wakali wanaomboleza na kulia. 11 Walakini hao waliposikia kama yu hai, naye amemwona, hawakusadiki.
12 Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba. 13 Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki.
14 Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. 15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. 16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. 17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; 18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.
19 Basi Bwana Yesu, baada ya kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni, akaketi mkono wa kuume wa Mungu. 20 Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo.
Maelezo ya teolojia
haririYesu alipokufa, nafsi yake ya Kimungu iliendelea kushikamana na roho na mwili vilivyotengana: kwa hiyo mwili wake uliozikwa haukuweza kuoza kaburini; roho yake ilishukia kuzimu kuwatoa waadilifu waliomtangulia awaingize pamoja naye mbinguni. “Mwili wake aliuawa, bali roho yake akahuishwa, ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiri” (1Pet 3:19). “Roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu” (Mdo 2:31).
Siku ya tatu roho ya Yesu ilirudi mwilini mwake na kudhihirisha utukufu wa ufufuko. Tangu mwanzo Wakristo wanakiri kwa ufupi “ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko” (1Kor 15:4).
Ufufuko wa Yesu siku ya Jumapili ulishuhudiwa na malaika waliowaambia wanawake waliofika kaburini: “Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Hayupo hapa, amefufuka” (Lk 24:5-6). Halafu Maria Magdalena, Petro na Mitume wenzake, hata watu zaidi ya mia tano walimuona na kumsikia, walimgusa na kula pamoja naye.
Yesu hakurudia maisha ya duniani: tofauti na watu aliowafufua warudie maisha haya, Yesu mfufuka ameshaingia utukufu wa milele: “amekwenda zake mbinguni” (1Pet 3:22), “hafi tena” (Rom 6:9), ana “funguo za mauti, na za kuzimu” (Ufu 1:18).
Ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa. Mwenyewe alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele” (Yoh 11:25-26). “Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu” (1Kor 15:20-21). “Alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa haki” (Rom 4:25).
Marejeo
hariri- Barrett, C.K. The Gospel According to John, 2nd Edition. London:SPCK, 1978.
- Brown, Raymond E. "The Gospel According to John: XIII-XI" The Anchor Bible Series Volume 29A. New York: Doubleday & Company, 1970.
- Bruce, F.F. The Gospel According to John. Grand Rapids: William B. Eerdmans Publishing Company, 1983.
- Catholic Encyclopedia, The resurrection of Jesus Christ
- Craig, William Lane, The Bodily Resurrection of Jesus
- Craig, William Lane, The Son Rises. 2001
- Kessler, Hans, La Risurrezione di Gesù Cristo. Uno studio biblico, teologico-fondamentale e sistematico, Queriniana, Brescia, 1999.
- Habermas, Gary, Overview of Dr. Habermas's analysis of 1 Corinthians 15:3-8
- Habermas, Gary, The Historical Jesus: Ancient Evidence for the Life of Christ (College Press: Joplin, MI 1996).
- Habermas, Gary and Licona, Michael, The Case for the Resurrection of Jesus. Kregel Publications, 2004.[1] Archived 30 Agosti 2008 at the Wayback Machine.
- Holding, James Patrick The Impossible Faith Archived 14 Mei 2011 at the Wayback Machine.
- Holding, James Patrick Broken Vector Sinks Again Archived 3 Oktoba 2006 at the Wayback Machine. (a reply to Richard Carrier)
- Leonard, W. "St. John." A Catholic Commentary on the Bible. D.B. Orchard ed. New York: Thomas Nelson & Sons, 1953.
- Vittorio Messori, Dicono che è risorto, S.E.I., 2000
- Antonio Persili, Sulle tracce del Cristo Risorto, C.P.R., 1988
- Schnackenberg, Rudolf . The Gospel According to St. John: Volume III. Crossroad, 1990.
- Williams, Rowan, Resurrection: Interpreting the Easter Gospel, 2003
- Westcott, B.F The Gospel of St. John. London: John Murray, 1889.
- Wenham, John. Easter Enigma: Do the Resurrection Stories Contradict One Another? Cambridge University Press, 1993.
- Wesley, John. The Wesleyan Bible Commnetary. Ralph Earle ed. Grand Rapids: William B. Eerdmans Publishing Company, 1964.
- Wright, N.T., Risurrezione, Claudiana, 2006 [2]
- Wright, N.T., Jesus’ Resurrection and Christian Origins Archived 20 Machi 2011 at the Wayback Machine.
- Wright, N.T., The New Testament and the People of God Fortess Press
- Wright, N.T., Jesus and the Victory of God Fortess Press
- Wright, N.T., The Challenge of Jesus: Rediscovering who Jesus was and is. IVP 1996
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ufufuko wa Yesu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |