Tirana
Tirana (Kialbania: Tiranë au Tirana) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Albania. Idadi ya wakazi imekadiriwa kuwa kati ya 350,000 (kadirio rasmi ya mwaka 2003) na milioni moja.
Jiografia
haririMji uko karibu na mlima Dajti (m 1611 juu ya UB) takriban km 30 kutoka mwabao wa Adria.
Madhehebu
haririKihistoria Tirana ilikuwa kasa mji wa Kiislamu wakati wa utawala wa Waturuki Waosmani. Kuna pia maaskofu wa kikristo wa kanisa orthodoksi na kanisa katoliki. Siku hizi kuna madhehebu yote kutokana na uhamiaji ndani ya nchi. Dini zote zilipigwa marufuku katika Albania wakati wa utawala wa ukomunisti hadi 1990. Maisha ya kidini imejengwa upya tangu kurudi wa uhuru huu. Tirana ni pia makao makuu ya jumuiya ya kiislamu ya Bektashi.
Historia
haririTirana ilianzishwa na Waosmani Waturuki mnamo 1614. Ikawa mji mkuu baada ya uhuru wa Albania mwaka 1920.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Tirana kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |