Jamhuri ya Albania ni nchi ya Ulaya Kusini Mashariki. Imepakana na Montenegro, Kosovo, Masedonia Kaskazini na Ugiriki. Upande wa magharibi kuna pwani ya ghuba ya Adria ya bahari ya Mediteranea.

Albania


Albania ni kati ya nchi zinazoendelea na imeomba kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Mji mkuu ni Tirana (wakazi 418,495).

Historia hariri

Historia ya kale hariri

Albania ilikaliwa na makabila mbalimbali ya Wailiriko, Wathraki na ya Wagiriki.

Katika karne ya 3 KK eneo lilitekwa na Dola la Roma na kufanywa sehemu ya majimbo ya Dalmatia, Masedonia na Iliriko.

Karne za Kati hariri

Mwaka 1190 ndani ya Dola la Roma Mashariki ulitokea ufalme mdogo wa Arbër kwa juhudi za archon Progon huko Krujë.

Mwishoni mwa karne ya 13 Charles wa Anjou aliwanyang'anya Wabizanti eneo hilo na kuanzisha Ufalme wa Albania kutoka Durrës hadi Butrint.

Katikati ya karne ya 15 nchi ilitekwa na Waosmani.

Historia ya kisasa hariri

Albania ya sasa ilitokea mwaka 1912, baada ya Waosmani kushindwa katika vita vya Balkani.

Ufalme wa Albania ulitekwa na Italia ya Benito Mussolini mwaka 1939 hadi 1943, ulipowekwa na Ujerumani wa Adolf Hitler chini yake.

Baada ya nchi hizo mbili kushindwa vitani, nchi ikaongozwa na Enver Hoxha ikijitenga zaidi na zaidi na dunia nzima.

Kati ya miaka 1945 na 1990 ilipotawaliwa na chama cha Kikomunisti Albania ilitangaza kuwa nchi ya kwanza ya kiatheisti na kupiga marufuku kila aina ya dini.

Kutokana na mapinduzi ya mwaka 1991 Jamhuri ya Kisoshalisti iliiachia nafasi jamhuri ya nne.

Kwa sasa Albania ni kati ya nchi maskini zaidi za Ulaya na wananchi wengi (walau 900,000) wamehamia Ugiriki, Italia, Marekani n.k.

Watu hariri

Wamebaki wakazi 2,876,591 (2017). Zaidi ya 98% za wakazi hutumia lahaja za Kialbania ambacho ni lugha ya pekee kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya. Lakini wengi wanazungumza pia Kigiriki au lugha nyingine.

Kati ya miaka 1945 na 1990 ilitawaliwa na chama cha Kikomunisti iliyotangaza Albania kuwa nchi ya kwanza ya kiatheisti iliyopiga marufuku kila aina ya dini. Hata hivyo, baada ya uhuru kupatikana tena, 39% za wakazi anajali sana imani fulani. Katika sensa ya mwaka 2011, 58.79% walijitambulisha kama Waislamu (hasa Wasuni) na 17.06% Wakristo (wakiwemo 10.03% Wakatoliki na 6.75% Waorthodoksi). Wakanamungu walikuwa 2.5% tu.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Albania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.