Tony Nyadundo
Tony Nyadundo ni mwana muziki nchini Kenya. Huimba muziki wa Ohangla ,mtindo wa kitamaduni wa kabila la waluo. Hushirikiana na bendi ya Ohangla Boys . Anatambulika sasa kama "Mfalme wa Ohangla".
Alizaliwa Kal nchini Tanzania. Dadake pacha alifariki Tony alipokuwa mchanga. Familia yake ilihamia Nyahera,Wilaya ya Kisumu , Kenya mwaka wa 1978 na kisha baadaye Kongoni katika Nzoia. Alisomea shule ya msingi ya Kongoni hadi mwaka wa 1985 kisha kuingia shule ya sekondari ya Bugembe masomo yake yalipokatizwa kwa ukosefu wa hela mwaka uliofuatia. Alifanya kazi kama fundi wa nguo hadi mwaka wa 1992. Alijaribu pia kuwa DJ. Ndugu yake Jack Nyadundo, aliunda kikundi kilichokuwa kikicheza muziki wa Ohangla , hatimaye Tony alijiunga na kikundi hiki baada ya mwaka wa 1996. Baadaye,aliunda kikundi chake na kurudi Tanzania kwa muda mfupi. Mnamo mwaka wa 1998,alihamia Wilaya ya Migori nchini Kenya alikowatumbuiza wakaazi wavuvi wa eneo hili. Alimuajiri Onyi Papa Jey, mpiga orutu ambaye kwa sasa ni mwanamuziki na amekuwa mwanamuziki mkuu. Mnamo mwaka wa 1999,alihamia Dandora mjini Nairobi lakini hukupata mafanikio kimuziki na kisha kuhamia Kisumu, ambako ndugu yake Jack alikuwa mwana muziki mashuhuri.[1].
Album yake ya kwanza Ayaki ilitolewa mwaka wa 2002. Huu ulikuwa mwanzo mpya katika uimbaji wake na alianza kufaidika kwa kuwa mwana muziki. Album yake ya pili iliitwa Kidi Oba e Toke , inayomaanisha "kupigwa mawe mgongoni". Jina hili lilitokana na tukio ambapo walishambuliwa na majangili wakiwa wanatumbuiza na kumpiga mpiga ngoma wake mgongoni. Watu wengine kadhaa waliumia[1].
Mwaka wa 2006 alitoa album iliyoitwa Obama . Jina lake lilitokana na Barack Obama, rais wa Marekani ambaye babake alitoka katika eneo moja na Nyadundo [2].
Katika Tuzo za Muziki za Kisima za 2007,alishinda katika kitengo cha muziki wa kitamaduni[3]. Alikuwa miongoni mwa Wakenya 100 wenye ushawishi mkuu kama ilivyichaguliwa na gazeti la The Standard mnamo Agosti 2007 [4][5].
Mnamo Oktoba 2009, alitoa album mpya Migingo , iliyotajwa kufuatia kisiwa kilichuleta mgogoro cha Kisiwa cha Migingo [6].
Tony anfahamika kwa midundo yake ya kuvuma kama vile, dawa ya mapenzi, Obama na zingine. Ametumbuiza katika nchi kadhaa kama vile, Ujerumani na Marekani[7].
Alikuwa ameoleka lakini walitalikiana mwaka wa 1994. Ako na watoto wawili kutoka ndoa hiyo [1].
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 Daily Nation, 7 Agosti 2009: King of Ohangla speaks
- ↑ The Standard, 25 Agosti 2006: Tony Nyadundo, Ohangla King Archived 2009-05-31 at Archive.today
- ↑ ^ Washindi wa Kisima Awards 2007
- ↑ The Standard, 21 Agosti 2007: 100 most influential Kenyans Archived 13 Oktoba 2007 at the Wayback Machine.
- ↑ The Standard, 21 Agosti 2007: 100 most influential Kenyans - Entertainment Archived 5 Juni 2009 at the Wayback Machine.
- ↑ The Standard, 2 Oktoba 2009: Nyadundo album launch Archived 16 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- ↑ The Standard, 7 Desemba 2008: Ohangla maestro spreads his wings Archived 5 Juni 2009 at the Wayback Machine.