Turris in Mauretania

Turris in Mauretania ni makazi ya kale ya Afrika Kaskazini ya Kirumi katika jimbo la Kirumi la Mauretania Caesariensis.[1] Eneo lake halijulikani lakini inaaminika kuwa liko Algeria ya leo.

Mauretania Caesariensis (125 BK)

Mji huu unaaminika ulikuwa na uaskofu,[2] lakini hakuna maaskofu wa zamani wanaojulikana kwetu.

Kiambishi "in Mauretania" ni kutofautisha mji huu na miji iliyokuwepo Hispania na majimbo ya jirani ya Afrika Kaskazini ya Kirumi.[3]

Dayosisi hii inabakia leo kuwa jimbojina la Kanisa Katoliki katika kanda ya Karthago. Askofu wa sasa wa kiheshima ni Askofu Alain de Raemy, askofu msaidizi wa Lausanne, Genève na Fribourg (Uswisi).[4]

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Turris in Mauretania kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.