Aljeria
Aljeria ni nchi ya Afrika ya Kaskazini-Magharibi. Imepakana na bahari ya Mediteranea, Moroko, Sahara ya Magharibi, Mauretania, Mali, Niger, Libya na Tunisia. Aljeria ni nchi kubwa kuliko zote za Afrika lakini sehemu kubwa ya eneo lake iko katika jangwa la Sahara.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Aljeria | |
---|---|
الجمهورية الجزائرية الديمقراطية الشعبية (Kiarabu) al-Jumhūriyah al-Jazāʾiriyah ad-Dīmuqrāṭiyah ash‑Shaʿbiyah | |
Kaulimbiu ya taifa: بِالشَّعْبِ و لِلشَّعْبِ "Biš-šaʿb wa liš-šaʿb" "Na watu, kwa watu" | |
Wimbo wa taifa: قَسَمًا Kasaman "Tunaapa" | |
Mahali pa Aljeria | |
Ramani ya Aljeria | |
Mji mkuu na mkubwa nchini | Aljeri |
Lugha rasmi | Kiarabu Kiberberi |
Makabila (asilimia) | 85 Waarabu 15 Waberberi |
Dini (asilimia) | 99 Wasuni (rasmi) |
Serikali | Jamhuri |
• Rais • Waziri Mkuu • Rais wa Baraza • Rais wa Bunge | Abdelmadjid Tebboune Nadir Larbaoui Salah Goudjil Ibrahim Boughali |
Idadi ya watu | |
• Kadirio la 2023 | 44 758 398[1] |
Pato la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 224.107[2] |
• Kwa kila mtu | USD 4 874[2] |
Pato halisi la taifa | Kadirio la 2023 |
• Jumla | USD bilioni 628.990[2] |
• Kwa kila mtu | USD 13 681[2] |
Maendeleo (2021) | 0.745[3] - juu |
Sarafu | Dinari ya Aljeria |
Majira ya saa | UTC+1 |
Muundo wa tarehe | siku/mwezi/mwaka |
Upande wa magari | Kulia |
Msimbo wa simu | +213 |
Msimbo wa ISO 3166 | DZ |
Jina la kikoa | .dz |
Jina
haririMajina mengine yake ni: الجزائر, al-Jazā’ir (Kiarabu); الدزاير, al-dzāyīr (Kiarabu cha Aljeria); ⴷⵣⴰⵢⴻⵔ, Dzayer (Kiberberi); Algérie (Kifaransa). Jina lake rasmi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Aljeria (Kiarabu: الجمهورية الجزائرية الديمقراطية الشعبية, al-Jumhūriyah al-Jazāʾiriyah ad-Dīmuqrāṭiyah ash‑Shaʿbiyah; Kifaransa: République algérienne démocratique et populaire).
Asili ya jina
haririJina la nchi limetokana na mji mkuu Aljeri unaoitwa kwa jina lilelile kwa Kiarabu al-Jazāʾir (الجزائر, "visiwa") linalohusu visiwa karibu na pwani yake. Aljeri iliitwa na Buluggin ibn Ziri.
Jiografia
haririSehemu kubwa ya nchi ni jangwa, Sahara iko upande wa kusini. Asilimia 20 za eneo la Aljeria upande wa kaskazini ni makao kwa karibu wakazi wote. Maeneo haya ni pwani ya Mediteranea na milima ya Atlas. Atlas inapanda hadi kimo cha mita 2,308 juu ya UB.
Sahara inaanza kusini kwa Atlas na kanda yenye nyasi chache, halafu inafuata eneo la matuta ya mchanga pasipo mimea yote. Kusini kwake tena ni nyanda za juu ambazo ni hasa maeneo ya miamba mitupu.
Kusini kabisa kuna milima kama Tassili n'Ajjer na Ahaggar inayopanda hadi mita 2,918 na kuwa kama visiwa vya uoto katika jangwa.
Mito ya kudumu iko kaskazini tu, sehemu za pwani. Mabonde ya mito ya ndani ni makavu, isipokuwa baada ya mvua mito mikali inajitokeza kwa masaa kadhaa.
Hali ya hewa
haririKanda la kaskazini lina hali ya hewa inayoathiriwa na Bahari ya Mediteranea. Huko halijoto kwenye mwezi Agosti ni 25 °C na 12 °C wakati wa Januari.
Kwenye sehemu za juu kuna baridi na hata barafu kwenye majira ya Januari lakini joto ni kali zaidi wakati wa Julai/Agosti.
Kusini ya Atlas inaanza hali ya hewa ya jangwani; halijoto inaweza kucheza zaidi ya 20 °C katika siku moja. Wakati wa joto halijoto inapita 40 °C lakini wakati wa baridi halijoto inashuka chini ya °C kwenye saa za usiku.
Mvua ni haba mno: kuna miaka mfululizo bila tone hata moja. Katika milima ya Ahaggar kuna usimbishaji kidogo kutokana na ukungu, kwa hiyo miti kadhaa na mimea mingine iko.
Historia
haririHistoria ya kale
haririHistoria inayojulikana ilianza na Waberber ambao wametokana na mchanganyiko wa wakazi asilia.
Tangu mwaka 1000 KK Wafinisia walianza kufika na kujenga miji yao ya biashara kwenye pwani ya Mediteranea. Muhimu zaidi kati ya miji yao ulikuwa Karthago uliopanua utawala wake hadi Hispania na Gallia (Ufaransa ya Kusini).
Kumbe Waberber wa bara walijenga milki zao za Numidia na Mauretania.
Katika vita kati ya Karthago na Roma ya Kale Waberber walisimama upande wa Roma, hivyo wakapata uhuru wao kwa muda kidogo, lakini wakati wa karne ya 1 KK Roma ilianza kutawala eneo la Aljeria moja kwa moja.
Numidia na Mauretania zilikuwa mashamba ya Roma na sehemu kubwa ya nafaka za Italia zililimwa huko.
Mawe ya maghofu ya miji ya kale bado yanaonyesha uhusiano wa Aljeria na Dola la Roma lililoitawala kwa karne nyingi hadi kuja kwa Waarabu katikati ya karne ya 7.
Utawala wa Roma ulivurugika baada ya Wavandali kutoka Ulaya Kaskazini kufika na kuanzisha milki yao kwa muda wa karne moja.
Jeshi la Kaisari Justiniani I wa Bizanti ilirudisha utawala wa Kiroma, ila tu katika karne ya 7 uvamizi wa Waarabu Waislamu ulimaliza kipindi cha Kiroma.
Uvamizi wa Waarabu
haririKuanzia mwaka 642 vikosi vya Waislamu Waarabu kutoka Misri walishambulia eneo la Afrika ya Kaskazini. Mwanzoni hawakufaulu kuwashinda Wabizanti lakini, baada ya uhamisho wa serikali ya makhalifa kutoka Medina kwenda Dameski, Waumawiya walikaza jitihada huko Afrika ya kaskazini.
Mwaka 670 jeshi kubwa la Waarabu likaunda mji wa Kairuan kusini ya Tunis ya leo na mji huu ulikuwa kitovu cha uenezaji. Walipoenea katika Aljeria ya leo walirudishwa na Waberber Wakristo kwa msaada wa Wabizanti lakini jeshi lililofuata lilishinda na kufikia mwaka 711 Afrika ya kaskazini yote (maana yake nchi za leo za Tunisia, Aljeria na Moroko) zilikuwa chini ya utawala wa Waarabu. Hapo sehemu kubwa ya Waberber walifanya haraka kujiunga na Uislamu wakasaidiana na Waarabu.
Matokeo hayo yalikuwa chanzo cha mabadiliko makubwa ya kudumu, maana yake upanuzi wa lugha ya Kiarabu kati ya wananchi na uenezaji wa Uislamu.
Ukoloni wa Wafaransa
haririHistoria ya karibuni imeacha kumbukumbu yake inayoonekana katika athira kubwa ya lugha na utamaduni wa Kifaransa kutokana na ukoloni wa Ufaransa kati ya miaka 1830 na 1962.
Kwa Marais wa nchi tangu uhuru, angalia Orodha ya Marais wa Aljeria.
Kwa sasa Aljeria inajenga upya umoja wa kitaifa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoishia mwaka 2002.
Nchi imebaki na idadi kubwa (25-30%) ya wakazi wa kabila la Waberber ambao kihistoria ndio wakazi asilia. Lakini kwa lugha, utamaduni na historia Aljeria ya leo ni sehemu ya dunia ya Kiarabu.
Wilaya za Aljeria
haririKuna vitengo vya utawala 48 vinavyoitwa wilaya, zinazolingana zaidi na mikoa katika nchi zingine.
|
|
|
|
Miji mikubwa
haririWatu
haririWakazi wengi wana mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na ya Kiberber na wachache ya Kituruki na ya Kiberber; karibu wote (98%) wanafuata dini ya Uislamu.
Wakristo ni 1%, wakiwemo Waprotestanti na Wakatoliki, lakini wengine wanashindwa kujitokeza kutokana na hofu ya dhuluma.
Lugha rasmi ni Kiarabu (72%) na Kiberber (27-30%), lakini wengi sana wanaongea pia Kifaransa.
Tazama pia
haririMarejeo
hariri- ↑ "Angola". The World Factbook (kwa Kiingereza) (tol. la 2024). Shirika la Ujasusi la Marekani. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 "World Economic Outlook Database, October 2023 Edition. (Algeria)". IMF.org. International Monetary Fund. 10 Oktoba 2023. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Data Futures Exchange (Algeria)". data.undp.org. Umoja wa Mataifa. Iliwekwa mnamo 23 Machi 2024.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Kujisomea
hariri- Ageron, Charles-Robert (1991). Modern Algeria – A History from 1830 to the Present. Translated from French and edited by Michael Brett. London: Hurst. ISBN 978-0-86543-266-6.
- Aghrout, Ahmed; Bougherira, Redha M. (2004). Algeria in Transition – Reforms and Development Prospects. Routledge. ISBN 978-0-415-34848-5.
- Bennoune, Mahfoud (1988). The Making of Contemporary Algeria – Colonial Upheavals and Post-Independence Development, 1830–1987. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 978-0-521-30150-3.
- Fanon, Frantz (1966; 2005 paperback). The Wretched of the Earth. Grove Press. ASIN B0007FW4AW, ISBN 978-0-8021-4132-3.
- Horne, Alistair (1977). A Savage War of Peace: Algeria 1954–1962. Viking Adult. ISBN 978-0-670-61964-1, ISBN 978-1-59017-218-6 (2006 reprint)
- Laouisset, Djamel (2009). A Retrospective Study of the Algerian Iron and Steel Industry. New York City: Nova Publishers. ISBN 978-1-61761-190-2.
- Roberts, Hugh (2003). The Battlefield – Algeria, 1988–2002. Studies in a Broken Polity. London: Verso Books. ISBN 978-1-85984-684-1.
- Ruedy, John (1992). Modern Algeria – The Origins and Development of a Nation. Bloomington: Indiana University Press. ISBN 978-0-253-34998-9.
- Stora, Benjamin (2001). Algeria, 1830–2000 – A Short History. Ithaca, New York: Cornell University Press. ISBN 978-0-8014-3715-1.
- Sidaoui, Riadh (2009). "Islamic Politics and the Military – Algeria 1962–2008". Religion and Politics – Islam and Muslim Civilisation. Farnham: Ashgate Publishing. ISBN 0-7546-7418-5.
Viungo vya nje
hariri- Serikali
- El Mouradia official presidential site (in French and Arabic)
- National People's Assembly official parliamentary site
- Chief of State and Cabinet Members Ilihifadhiwa 29 Juni 2011 kwenye Wayback Machine.
- Maelezo zaidi
- Algeria entry at The World Factbook
- Algeria Ilihifadhiwa 13 Aprili 2016 kwenye Wayback Machine. from UCB Libraries GovPubs
- Aljeria katika Open Directory Project
- Wikimedia Atlas of Algeria
- Algeria travel guide kutoka Wikisafiri
- Photos From Algeria
- Ministère de l'Aménagement du Territoire, de l'Environnement et du Tourisme Ilihifadhiwa 18 Machi 2009 kwenye Wayback Machine.
- Map of Algeria Ilihifadhiwa 27 Machi 2014 kwenye Wayback Machine.
Nchi za Afrika | |
---|---|
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe | |
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika | |
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira |
Makala hii kuhusu maeneo ya Algeria bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Aljeria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |