Tuzo ya Sao Paulo ya Fasihi

Tuzo ya Sao Paulo ya Fasihi (kwa Kireno: Prêmio São Paulo de Literatura) ni tuzo ya fasihi ya Brazil ambayo hutolewa kwa ajili ya riwaya zilizotungwa kwa lugha ya Kireno na kuchapishwa nchini Brazil. Tuzo hii ilianzishwa mnamo mwaka wa 2008 na Waziri wa Utamaduni wa Jimbo la São Paulo. Ijapokuwa si la kale sana kama jinsi zilivyo tuzo zingine za fasihi huko nchini Brazili kama Prêmio Machado de Assis.

Tuzo hii ya São Paulo imechupukia haraka zaidi na kupata sifa kubwa mno. Kwa mfano, mwaka wa 2011, kulikuwa na mawasilisho 221 kwa ajili ya ugawaji wa tuzo.[1]

Washindi hariri

Mwaka Kitabu Bora ya Mwaka Kitabu Bora ya Mwaka - Mwandishi Chipukizi
Kichwa Mtunzi Kichwa Mtunzi
2008 O Filho Eterno Cristóvão Tezza A Chave de Casa Tatiana Salem Levy
2009 Galiléia Ronaldo Correia de Brito A Parede no Escuro Altair Martins
2010 A minha alma é irmã de Deus Raimundo Carrero Se eu fechar os olhos agora Edney Silvestre
2011 Passageiro do Fim do Dia Rubens Figueiredo Método Prático da Guerrilha Marcelo Ferroni
2012 Vermelho Amargo Bartolomeu Campos de Queirós Os Hungareses Suzana Montoro

Marejeo hariri

  1. R$200,000 São Paulo Literary Award Shortlist Announced. Publish News Brazil. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-07-21. Iliwekwa mnamo 16 March 2013.