Uapolinari
Uapolinari ni fundisho la Apolinari wa Laodikea (alifariki mwaka 390) kwamba Yesu hakuwa na akili ya kibinadamu; badala yake alisema Yesu Kristo alikuwa na mwili na upande wa chini tu wa roho (zinapotokea hisia) lakini akili yake ilikuwa ya Kimungu.
Inaonekana alifundisha hivyo katika juhudi za kupinga Uario uliokanusha umungu wa Yesu.[1]
Baada ya kupingwa na Theodoreto wa Kuro na Basili Mkuu, fundisho hilo lililaaniwa na Sinodi ya Aleksandria ya mwaka 362, iliyoongozwa na Atanasi wa Aleksandria, na hatimaye kutajwa kama uzushi na Mtaguso wa kwanza wa Konstantinopoli (381), uliosisitiza kwamba Kristo ni Mungu kamili na mtu kamili.
Tanbihi
hariri- ↑ McGrath, Alister. 1998. Historical Theology, An Introduction to the History of Christian Thought. Oxford: Blackwell Publishers. Chapter 1.
Marejeo
hariri- Catholic Encyclopedia entry
- Artemi, E., «Mia physis of God Logos sesarkomeni» a)The analysis of this phrase according to Cyril of Alexandria b)The analysis of this phrase according to Apollinaris of Laodicea»,Ecclesiastic Faros t. ΟΔ (2003), 293 – 304.
- McGrath, Alister. 1998. Historical Theology, An Introduction to the History of Christian Thought. Oxford: Blackwell Publishers. Chapter 1.
- Edwards, Mark (2009). Catholicity and Heresy in the Early Church. Ashgate.
{{cite book}}
: Invalid|ref=harv
(help)
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Uapolinari kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |