Uche Elendu

Muigizaji na Muimbaji wa kike kutoka Nigeria

Uche Elendu (alizaliwa 14 Julai 1986) ni mwigizaji, mwimbaji na mjasiriamali[1] wa kike kutoka nchini Nigeria [2].

Alifafanuliwa kama mmojawapo wa waigizaji wenye sura thabiti katika tasnia ya sinema ya Nigeria. Kutokea kwake kwa mara ya kwanza ni mnamo mwaka 2001. Mwaka 2010 alichukua mapumziko kutoka tasnia ya burudani ya Nigeria. Kulingana na machapisho ya Vanguard, Elendu ameshiriki zaidi ya sinema 200 za kinigeria. [2][3][4]

Maisha ya awali hariri

Elendu alizaliwa katika jimbo la Abia, kusini mashariki mwa Nigeria, ambapo ni makazi ya watu wa kabila la Igbo. Elendu ni mzaliwa wa kwanza katika familia yao na ana wadogo zake watatu wote wa kiume. Baba yake ni mstaafu wa serikali pia mjasiriamali na mama yake ni mwalimu.Elendu alihitimu chuo kikuu cha Imo State University na kupata shahada ya uhusiano wa kimataifa.[5]

Kazi hariri

Elendu alijiunga rasmi na tasnia ya filamu ya nchini Nigeria mwaka 2001. Alianza kazi yake ya uigizaji kwa kushiriki katika filamu inayofahamika kwa jina la Fear of the Unknown.Elendu kutokana na ndoa alichukua mapumziko marefu katika uigizaji ambapo hatua hii ilimharibia kazi yake ya kuigiza. Mwaka 2015 alirudi katika kazi ya uigizajina kua mshiriki mkuu katika filamu inayo famika kwa jina la Ada Mbano.Filamu hii ilikua kichocheo katika kazi yake.

Katika moja ya mahojiano na The Sun ya nchini Nigeria, Elendu alielezea tabu alizopata kurudi katika tasinia ya uigizaji baada ya kuchukua likizo ya mda mrefu. Alielezea uhusika wake katika filamu ya Ada Mbano na jinsi ilivyokua na mchango chanya katika kazi yake. Wakati wa mahojiano, alielezea kwa ufupi mchango wa filamu hiyo kwa kusema “Filamu iliyonirudisha mimi ni ya Ada Mbano”.

Maisha binafsi hariri

Elendu, japokuwa kwa sasa ana talaka, aliolewa mwaka 2012 na bwana Ogochukwu Igweanyimba mjini Owerri, Imo, na kupata watoto wawili wa kike[6]. Elendu alipata ajali ya barabarani ambapo mojawapo ilimfanya apoteze fahamu.[7][8]

Afya hariri

Elendu aliweka wazi kuhusu tatizo la kiafya alilokua nalo kwa jina Endometriosisi.[9][10][11]

Filamu zilizochaguliwa hariri

  • Nigerian Girls (2009)
  • The Rain Makers (2009)
  • Twilight SIsters (2009)
  • Angelic Bride (2008)
  • Bottom Of My Heart (2008)
  • Don’t Wanna Be A Player (2008)
  • Give It Up (2008)
  • Yankee Girls (2008)
  • Beyond The Verdict (2007)
  • Johnbull & Rosekate (2007)
  • Lost In The Jungle (2007)
  • Missing Rib (2007)
  • Most Wanted Bachelor (2007)
  • Mountains Of Evil (2007)
  • Old Testament (2007)
  • Before Ordination (2007)
  • Brain Wash (2007)
  • Chicken Madness (2006)
  • Holy Cross (2006)
  • Return Of The Ghost (2006)
  • Occultic Battle (2005)
  • Omaliko (2005)
  • Security Risk (2005)
  • To Love And Live Again (2005)
  • Woman On Top (2005)

Marejeo hariri

  1. "How women can tie down their hubbies –Uche Elendu, actress". The Sun Nigeria (kwa en-US). 2019-10-20. Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  2. 2.0 2.1 "See Uche Elendu sexy birthday photoshoot". Vanguard News (kwa en-US). 2015-07-15. Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  3. "Beans and plantain reminds me of childhood – Uche Elendu". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  4. "Money we make in movies doesn't match the effort – Uche Elendu". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  5. "I'd be worried if men don't make passes at me -Uche Elendu". Punch Newspapers (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  6. "What fame has denied me – Uche Elendu, actress". The Sun Nigeria (kwa en-US). 2017-11-12. Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  7. "Uche Elendu I would have been dead". The Sun Nigeria (kwa en-US). 2018-01-20. Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  8. sunnews (2017-09-10). "My unforgettable car accident – Uche Elendu, actress". The Sun Nigeria (kwa en-US). Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  9. "Uche Elendu Actress opens up about her struggle with endometriosis". www.pulse.ng. Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  10. Helen, Ajomole (2017-04-27). "How I went through 7 years of severe pain - Top actress shares powerful testimony (photos)". www.legit.ng (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-12-09. 
  11. "Nollywood Actress Uche Elendu Celebrates Her Miracle Baby After Surviving Endometriosis".  Unknown parameter |url-status= ignored (help)
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uche Elendu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.