Umande
Umande (pia: unyevu, ukungu; kwa Kiingereza: dew) ni maji yaliyo katika mfumo wa vijitone vionekanavyo juu ya vitu, hasa mimea, wakati wa asubuhi kutokana na utoneshaji na baridi.
Wakati halijoto ni ya chini vya kutosha umande huchukua umbo la barafu liitwalo sakitu. Kwa kuwa umande unategemeana na halijoto ya nyuso za vitu, mwishoni mwa msimu wa joto, umande hujitokeza kwa urahisi kwenye nyuso ambazo hazijatiwa joto kutoka chini ardhini kama vile nyasi, majani, mataruma ya reli, paa za magari na madaraja.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Umande kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |