Daraja ni jengo lililoundwa kwa kusudi la kuwa na njia ya kupitia juu ya pengo au kizuizi. Mfano mzuri ni daraja linaloendeleza barabara juu ya mto, bopo au juu ya barabara nyingine.

Daraja juu ya mto huko Hispania.

Kuna aina nyingi za madaraja. Ukubwa wa daraja unategemea upande mmoja upana wa kizuizi kinachotakiwa kuvukiwa, yaani upana wa mto au bopo, na kwa upande mwingine uzito wa mizigo itakayopita juu ya daraja. Daraja la kuvukisha watu halina mzigo mkubwa lakini daraja linalopokea njia ya reli au barabara kuu litabeba uzito mkubwa.

Kuna pia madaraja yanayovusha mfereji juu ya mto hivyo kuwezesha meli kupita juu ya meli nyingine. Kwa jumla madaraja ni sehemu muhimu za miundombinu ya kila nchi.

Upande wa kusini wa daraja la Lake Pontchartrain

Historia

hariri
 
daraja

Madaraja ya kwanza yalitengenezwa kwa mbao. Baadaye watu waliendelea kutumia mawe. Tangu karne ya 18 madaraja ya chuma yalianza kujengwa. Baadaye madaraja mengi yamejengwa kwa kutumia saruji pamoja na feleji.

Madaraja marefu duniani

hariri

Daraja refu zaidi duniani ni Bang Na Expressway mjini Bangkok (Uthai) lenye urefu wa kilomita 54. Linapitisha barabara kuu ya mpito juu ya eneo la jiji.

Daraja refu la pili ni Lake Pontchartrain Causeway linalovuka ziwa Pontchartrain karibu na mji wa New Orleans (Marekani) lenye urefu wa kilomita 38. Madaraja haya yanasimama juu ya nguzo zinazokaa karibu kwa sababu nafasi ya chini si ngumu.

Daraja linaloning'ania

hariri
 
Daraja linaloning'ania la Akashi

Ugumu wa kujenga daraja ni kuwa zaidi kama nafasi ya kuvukia ni mkono wa bahari na maji yana kina kikubwa. Hapo haiwezekani kuwa na nguzo nyingi na hapa aina ya daraja linaloning'inia inatumiwa. Daraja kubwa linaloning'ania duniani ni daraja la Akashi-Kaikyo (Japani) lenye upana wa kilomita 2 kati ya nguzo za katikati.

Aina za madaraja juu ya njia ya maji

hariri
 
Daraja la kukunjwa
 
Daraja linalopandishwa
 
Daraja linalogeuzwa
 
Daraja la mfereji kuvuka mto
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Daraja kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: