Umemenuru
Umemenuru (pia: umeme-mwanga, fotovoltaiki, kutoka Kiingereza photovoltaics, photoelectricity) ni umeme unaopatikana kutokana na nishati ya nuru hasa au kwa jumla kila aina ya mnururisho wa sumakuumeme. Badiliko hili linatokea katika seli zinazojulikana mara nyingi kama seli za sola. Seli ya umemenuru inatoa mkondo wa takriban nusu volti.
Nishati ya nuru ikikuta mata yenye tabia ya nusukipitishi (semikonda) inasababisha mwendo wa elektroni ndani yake. Nuru inaundwa na vipande vidogo vinavyoitwa fotoni. Nishati ya fotoni ikigonga elektroni inaweza kuiondoa katika nafasi yake kwenye mzingo elektroni na kusababisha kutokea kwa mkondo wa umeme.
Matumizi ya umemenuru yanapatikana katika teknolojia ya umemejua kwa uzalishaji wa umeme, lakini pia kwa vihisio (sensor) vya aina , mfano katika kamera au vifaa vya kupimia umbali, mwendo na kadhalika.
Marejeo
hariri
Viungo vya nje
hariri- What is Photovoltaics?, tovuti ya NASA, iliangaliwa Machi 2019
- Godwin Msigwa: Mafunzo ya umeme wa jua , tovuti ya dtpev.de, iliangaliwa Machi 2019
- How do solar panels work?, tovuti ya livescience.com, imeangaliwa Machi 2019
- Basic Photovoltaic Principles and Methods, tovuti ya National Renewable Energy Laboratory, Marekani, iliangaliwa Machi 2019
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Umemenuru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |