Kifaa

(Elekezwa kutoka Vifaa)

Kifaa (kutoka kitenzi "kufaa") ni kitu chochote ambacho kinaweza kutumika kufikia lengo fulani.

Vifaa viwili.
Vifaa mbalimbali vinavyotumika tangu muda mrefu kwenye maisha ya kila siku.

Zana zinazotumiwa na wanadamu katika kurahisisha kazi au shughuli zao katika eneo fulani zinaweza kuwa na sifa tofauti kama "chombo", "mashine" au "kifaa".

Baadhi ya mifano ya zana ambazo mara nyingi hutumiwa leo ni kisu, nyundo, bisibisi, koleo, simu na kompyuta.

Seti ya zana zinazohitajika kufikia lengo ni "vifaa". Maarifa ya kutengeneza, kupata na kutumia zana ni teknolojia.

Kuna wanyama wengine ambao hutumiwa na watu kama kifaa, kwa mfano siafu katika kutibu vidonda.

Matumizi ya zana huchangia utamaduni wa binadamu na yalikuwa muhimu tangu kale.

Katika maisha ya sasa huwezi ukafanya kitu bila kutumia kifaa au vifaa.