Unafiki ni utovu wa ukweli katika mwenendo wa binadamu hasa kwa lengo la kujipatia sifa, k. mf. kama mwanadini mwadilifu.

Tofauti na mkosefu, mnafiki anatenda vema kwa nje, lakini nia yake si kufuata dhamiri yake na maadili anayojua ni mazuri, bali ni kupendeza watu wengine ili kupata faida fulani kutoka kwao.

Ni jambo linalolaumiwa sana katika dini zote, hasa Ukristo, kutokana na lawama za Yesu dhidi ya viongozi wengi wa Uyahudi. Injili zinasisitiza hasa lawama zake dhidi ya baadhi ya Mafarisayo.

Nuvola apps bookcase.svg Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Unafiki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.