Dhamiri ni kipawa cha binadamu kinachomwezesha kuamua kuhusu uadilifu au uovu wa tendo fulani analolikabili au alilolitenda.

Dhamiri hiyohiyo inamsukuma daima kutenda lililo adilifu na kukwepa lililo ovu.

Katika falsafa ya maadili wengi wanakubali kwamba uamuzi wa dhamiri unategemea ukweli ambao upo nje ya mhusika na ambao yeye anatakiwa kuutambua.

Baadhi ya wataalamu wa elimunafsia wanashika msimamo kuwa uamuzi wa dhamiri unategemea zaidi malezi na mang'amuzi ya mtu.

Katika dini, Ukristo unatia maanani sana dhamiri iliyozungumziwa na mtume Paulo kama sheria ya ndani ya mtu.

Mtaguso wa pili wa Vatikano ulifundisha: Ndani mwa dhamiri binadamu anakuta sheria anbayo hajipatii, bali anapaswa kuitii na ambayo sauti yake, inayomuita daima apende na kutenda maadilifu na kukimbia maovu inapotakiwa, inasema wazi katika masikio ya moyo wake [...]. Kwa kweli mtu ana sheria iliyoandikwa na Mungu katika moyo wake [...]. Dhamiri ni kiini cha siri zaidi na patakatifu pa mtu, ambapo anabaki peke yake na Mungu, ambaye sauti yake inasikika kwa ndani kabisa (Gaudium et Spes 16).

Viungo vya njeEdit