Unyayo (au uwayo) ni sehemu ya mwisho wa mguu unapokanyaga chini. Unatumika wakati wa kutembea na kusimama wima. Watu pia huutumia kwa teke, katika mapigano na michezo, mpira wa miguu ukiwa mfano mmojawapo. Unyayo pia ni dalili katika mchanga au matope.

Unyayo.
Mifupa katika mguu wa chini na mguu.

Kiganja na unyayo wa mtu hufanana na kuwa na muundo sawa. Vyote huwa na vidole vitano. Wanyama wengi walio na uti wa mgongo pia wana vidole vitano. Sehemu ya unyayo unaouunganisha na mguu inaitwa kisigino.

Unyayo wa wanyama kama ng'ombe huitwa kanyagio au kwato.

Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Unyayo kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.