Upasteurishaji
Upasteurishaji ni mbinu wa kutunza vyakula visiharibike haraka. Mbinu huu umeitwa kufuatana na mwanasayansi Mfaransa Louis Pasteur aliyeugundua mwaka 1862.
Vyakula kwa mfano maziwa hupashwa joto kiasi cha 70-90 °C kwa muda mfupi. Kwa njia hii sehemu kubwa ya vijidudu au vidubini kama bakteria ndani yake inauawa. Uharibifu wa chakula husababishwa na na vidubini hivi. Lakini joto la muda mfupi hautoshi kubadilisha sana ladha au sifa nyingine za vyakula.
Kama chakula unatunzwa baadaye katika chombo bila hewa pamoja na na vidubini vya hewani kuingia hakuna uharibifu mpya unaoweza kutokea. Lakini mbinu wa Pasteur hauui vidubini vyote kwa hiyo bado vyakula hivi vinaanza kuharibika lakini baada ya muda mrefu kulingana na kutopasha moto.
Vyakula vinavyouzwa ilhali vimepata upasteurishaji ni hasa vinywaji kama vile maziwa, maji ya matunda, bia, au divai. Maziwa iliyopasteurishwa ikitunzwa ndani ya chombo chake inakaa kwenye friji kwa muda wa siku 5-7. Lakini muda huu unategemea kama baridi imetunzwa kweli kwenye hatua zote kati ya kiwanda, duka na nyumbani. Kama maziwa imekaa kwenye joto au kubebwa kwenye gari katika mazingira ya joto uharibifu unaweza kutokea haraka zaidi.