Louis Pasteur
Louis Pasteur (27 Desemba 1822 – 28 Septemba 1895) alikuwa mwanasayansi kutoka Ufaransa. Aliweka misingi ya mikrobiolojia yaani utaalamu wa viumbe vidogo sana ambavyo huonekana kwa hadubini tu.
Pamoja na mke wake alifanya utafiti ulioonyesha ya kwamba mara nyingi magonjwa yanasababishwa na vidubini kama vile bakteria.
Aliendelea kugundua njia za kuongeza kinga cha mwili dhidi ya magonjwa kwa njia ya chanjo, akagundua chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa na kimeta.
Aligundua pia mbinu ya kutunza vyakula kama maziwa kwa muda mrefu na mbinu hiyo huitwa upasteurishaji kwa heshima yake. Kuharibika kwa vyakula kunazuiliwa kwa kupasha vyakula joto kiasi cha 70 °C na kuvifunga katika chombo bila hewa kuingia.
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Viungo vya nje
haririMakala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Louis Pasteur kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |