Usimulizi wa habari
Usimulizi wa habari ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani.
Mambo uhimu katika usimulizi wa habari
hariri- Aina ya tukio - msimuliaji anatakiwa kubainisha katika maelezo yake aina ya tukio.
- Mahali pa tukio - ili msikilizaji aweze kuelewa ile habari lazima msimuliaji aweze kumuelewesha tukio lilifanyika/lilitendeka sehemu gani.
- Wakati/muda - katika usimulizi ni muhimu pia kutaja tukio lilifanyika muda gani.
- Wahusika wa tukio - ni muhimu kutaja tukio lilifanywa na watu gani, jinsia zao, wingi wao, umri wao n.k.
- Chanzo cha tukio - ni muhimu kujua chanzo/vyanzo vya tukio, yaani tukio lilifanyajwe na chanzo chake ni nini.
- Athari za tukio - athari za tukio nazo ni sharti zibainishwe.
- Hatima ya tukio - msimuliaji ni lazima abainishe hatima ya tukio, yaani baada ya tukio kilifanyika kitu gani.
Misingi ya usimulizi wa habari
haririKuna misingi mitatu ya usimulizi wa habari:
- 1. utangulizi
- 2. kiini
- 3. mwisho.
Utangulizi
haririSehemu hii huwa na maelezo tu ya utangulizi ili kuvuta hisia na umakini wa msikilizaji/wasikilizaji.
Kiini
haririNi sehemu ambayo hueleza tukio halisi kuanzia chanzo chake, wahusika, mahali na athari za tukio.
Mwisho
haririNi matokeo yanayoonyesha mwisho wa usimulizi wa habari.
Mbinu za usimulizi
hariri- Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia sarufi na lafudhi sahihi ya Kiswahili au lugha nyingine yoyote.
kwa upande wa uigizi msimuliji atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio ambalo anasimulia.nayo ni kama vile mlio,sauti au vitendo.
kwa upande wa usimulizi ambao una fanyika kwa njia ya maandisha sharti usimulizi huo uwe na kichwa cha habari.kichwa cha habari kinatakiwa kisizidi maneno matano,yalioandikwa kwa herufi kuba.
kwa vile usimulizi wa tukio huwa unagusu tukio lilopita,maelezo yake mengi huandikwa wakati uliopita.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Usimulizi wa habari kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |