Uwanja wa michezo Nyayo

Uwanja wenye matumizi mengi uliopo Nairobi, Kenya
(Elekezwa kutoka Uwanja wa Nyayo)

Uwanja wa Taifa wa Nyayo ni uwanja unaotumika katika matumizi mbalimbali ya michezo na unapatikana katika jiji la Nairobi nchini Kenya. Umejengwa katikati ya barabara ya Mombasa . Barabara ya Langata na Barabara ya Aerodrome . Ni takribani kilometa mbili kutoka katikati ya Jiji, pia ni moja mkabala na Nairobi Mega Mall, zamani palijulikana kama Nakumatt Mega. Uwanja huo ulijengwa mnamo mwaka 1983 unachukua Takribani watu 30,000.( Elfu thelathini ) Hivi sasa unatumiwa zaidi na [[chama cha mpira wa miguu kwa kuchezesha mechi mbalimbali. Klabu maarufu ya AFC Leopards hucheza michezo yake ya nyumbani kwenye uwanja wa Nyayo. Uwanja huo pia hutumiwa kwa michezo ya riadha, kuogelea na sherehe za Kitaifa na kimataifa . Rasilimali nyingine zilizopo uwanja wa Nyayo ni pamoja na ukumbi wa mazoezi na dimbwi la kuogelea la mita 50. Klabu ya umoja wa raga Mwamba RFC pia Ulitumia Uwanja wa Kitaifa wa Nyayo kwa michezo ya nyumbani.

Uwanja wa michezo Nyayo

Kukamilika kwa Uwanja wa Nyayo kuliipa Kenya nafasi ya kuwekwa kwenye kitengo cha kuwania kuandaa michezo minne ya Afrika All-Africa Games mnamo mwaka 1987.

Badae uwanja ulibadilisha jina na kuitwa uwanja wa kitaifa wa Coca-Cola[1]

Viungo vya Nje

hariri

Marejeo

hariri
  1. "Nyayo National Stadium renamed in $1.5M". various. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Julai 2011. Iliwekwa mnamo 4 Februari 2009.
  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo Nyayo kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.