Uwanja wa michezo wa Amakhosi
Uwanja wa Amakhosi ni uwanja uliotazamiwa kuwa uwanja wa nyumbani kwa timu ya Afrika ya Kusini ya Kaizer Chiefs FC. Uwanja huu ungekuwa miongoni mwa viwanja bora vya michezo huko Krugersdorp, umbali wa kilomita 40 magharibi mwa Johannesburg. Hapo awali, uwanja huu ulitazamiwa kuwa uwanja wa kriketi, raga, hoteli ya michezo na duka la rejareja na sio kuwa ya Kaizer Chief na timu ya vijana ya Kaizer Chief pekee. Utengenezwaji wa uwanja huu ulipangwa kuanza mwezi Septemba mwaka 2006 kwa gharama ya R695 milioni.
Mwishoni mwa mwaka 2006, gharama ya mradi huu ulipandishwa na kufikia R1.2 billioni kutokana na matakwa na uhitaji wa Kaizer Chiefs kifikia viwango vya FIFA.
Mnamo Agostimwaka 2010, Kaizer Chiefs walitangaza ya kuwa mradi huo uliundwa upya kwa lengo la kupunguza gharama za kutengeneza na pia kufanikisha upatikanaji wa fedha ili matengenezo yaanze Septemba 2010 na kumalizika Agosti 2012. Kama muundo mpya uliopitiwa mnamo Aprili 2010 ungepitishwa na Kaizer Chiefs, uwanja huo mpya unge gharimu kiasi cha R700 milioni na uwezo wa kubeba watu ungepungua kutokea 55,000 hadi 35,000. Kutokana na uhaba wa fedha, mradi huo haukuanza.
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Amakhosi kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |