Agosti

mwezi wa nane katika mwaka
Jul - Agosti - Sep
1 2 3 4 5 6 7
8 9 10 11 12 13 14
15 16 17 18 19 20 21
22 23 24 25 26 27 28
29 30 31
Kalenda ya Gregori

Mwezi wa Agosti ni mwezi wa nane katika Kalenda ya Gregori. Jina lake limetokana na jina la Kaisari Augustus wa Warumi. Kwa asili, mwezi huo wa Agosti ulikuwa mwezi wa sita katika kalenda ya Warumi, na jina lake lilikuwa Sextilis kulingana na neno la Kilatini sextus, maana yake ni "wa sita". Mwaka wa 153 KK, mwanzo wa mwaka ulitanguliza miezi miwili kutoka Machi kwenda Januari, na maana ya jina Sextilis ilipotea.

Agosti ina siku 31, na katika mwaka mrefu (wenye siku 366), inaanza na siku ya juma sawa na mwezi wa Februari.

Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: