Uwanja wa michezo wa mwana mfalme Moulay Abdallah
Uwanja wa wa michezo wa mwana mfalme Moulay Abdellah ni uwanja wa michezo unaopatikana hukoRabat, nchini Moroko na ulipewa jina la mwana mfalme Moulay Abdellah wa Moroko.
Ilijengwa mnamo 1983 na ndio uwanja wa nyumbani wa ASFAR . Kwa sasa inatumiwa zaidi mpira wa miguu na unaweza pia kutumika katika riadha. Uwanja huu una uwezo wa kubeba washabiki 53,000.
Tangu 2008 umekuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa Mohammed VI d'Athlétisme de Rabat. Ulikuwa uwanja uliothibitishwa kuchezewa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2015 hadi Moroko iliponyang'anywa haki zake za kuwa mwenyeji. Moroko iliomba Kombe la Mataifa ya Afrika iahirishwe kwa sababu ya hofu ya janga la Ebola wakati huo lililoathiri nchi zingine za Kiafrika. Nchi hiyo ilikataliwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa. Uwanja wa mwana mfalme Moulay Abdellah pia ulikuwa uwanja wa Kombe la Dunia la FIFA ya 2014. Uwanja huu ulipangwa kuwa moja ya viwanja vya wenyeji kwa zabuni iliyoshindikana kuandaa Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2026. Ilikusudiwa kuandaa mechi za Robo Fainali ikiwa Moroko Ungepewa Kombe la Dunia. Sasa unajipanga kama mahali kuandaa Kombe la Dunia la FIFA ya mwaka 2030, wakati Moroko inaandaa zabuni yake wakishirikiana na Ureno na Uhispania. Ikiwa hili litatokea itakuwa zabuni ya kwanza ya mseto kwa zaidi ya bara moja. Itatumika pia kama uwanja wa sherehe ya ufunguzi na kufunga kwa Michezo ya Afrika ya mwaka 2019 baada ya Malabo, Guinea ya Ikweta kuondoa haki zake za kuandaa Michezo ya Afrika.
Marejeo
haririViunga vya nje
hariri- Picha kutoka fussballtempel.net