Vaginosisi inayosababishwa na bakteria
Vaginosisi inayosababishwa na bakteria (kifupisho cha Kiingereza: BV; pia inajulikana kama bakteriosisi ya uke au Vaginitisi ya gadinerela,[1] ni ugonjwa wa uke unaosababishwa na wingi wa bakteria.[2]
Vaginosisi inayosababishwa na bakteria | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Gynaecology |
ICD-10 | B96., N76. |
ICD-9 | 616.1 |
MeSH | D016585 |
Dalili za kawaida ni pamoja na ongezeko la mchozo wa uke ambao mara nyingi hutoa harufu ya samaki. Mchozo huu huwa wa rangi nyeupe au ya kijivu. Kuchomwa na mkojo ni hali inayoweza kutokea.[3] Kuwashwa huwa kwa nadra.[2][3] Mara kwa mara, hali hii huwa bila dalili.[3]
Uwepo wa BV huongeza hatari ya maambukizi ya maradhi ya zinaa ikiwa ni pamoja na VVU/UKIMWI.[4] Hali hii pia huongeza hatari ya kujifungua kabla ya wakati miongoni mwa wanawake wajawazito.[5]
Kisababishi na utambuzi
haririBV husababishwa na ukosefu wa uwiano wa bakteria asilia ukeni.[6] Kuna mabadiliko katika aina ya bakteria inayotokea mara nyingi zaidi na ongezeko la mia hadi elfu moja ya idadi jumla ya bakteria zilizopo.[2] Vipengele vya hatari hujumuisha kupiga bomba, wapenzi wapya au wengi, antibiotiki, na kutumia kifaa cha kuingiza ndani ya uterasi.[6] Hata hivyo, ugonjwa huu hauainishwi kama ugonjwa wa zinaa.[7] Utambuzi hukisiwa kwa msingi wa dalili na unaweza kuthibitishwa kwa kupima mchozo wa uke na kutambua viwango vya juu kuliko kawaida vya pH ya ukeni na idadi kubwa ya bakteria.[2] Mara nyingi BV hudhaniwa kuwa maambukizi ya chachu ya ukeni au maambukizi ya Trikomonasi.[8]
Kinga na tiba
haririKwa kawaida, matibabu huwa ya antibiotiki, clindamycin au metronidazole. Dawa hizi pia zinaweza kutumika katika trimesta ya pili au ya tatu ya ujauzito. Hata hivyo, mara nyingi hali hii hurejea baada ya kutibiwa. Probiotiki zinaweza kusaidia kuzuia kurejea kwa hali hii.[2] Haijulikani bayana kama kutumia probiotiki au antibiotiki huathiri matokeo ya ujauzito.[2][9]
Epidemiolojia na historia
haririBV ni maambukizi ya uke yanayotokea mara nyingi katika wanawake wa umri wa kuzaa.[6] Idadi ya wanawake wanaoathiriwa katika muda fulani ni kati ya asilimia 5 na asilimia 70.[4] BV hutokea mara nyingi zaidi katika maeneo mengi ya Afrika na ni nadra barani Asia na Ulaya.[4] Nchini Marekani, takriban asilimia 30 ya wanawake wa umri wa kati ya miaka 14 na 49 huathiriwa.[10] Viwango hutofautiana sana katika makundi ya kikabila mbalimbali katika nchi.[4] Ingawa BV kama dalili imeainishwa katika kipindi kirefu cha historia, nakala za kwanza bayana ziliwekwa katika mwaka wa 1894.[1]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Borchardt, Kenneth A. (1997). Sexually transmitted diseases : epidemiology, pathology, diagnosis, and treatment. Boca Raton [u.a.]: CRC Press. uk. 4. ISBN 9780849394768.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Donders, GG; Zodzika, J; Rezeberga, D (Aprili 2014). "Treatment of bacterial vaginosis: what we have and what we miss". Expert opinion on pharmacotherapy. 15 (5): 645–57. PMID 24579850.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 3.2 "What are the symptoms of bacterial vaginosis?". http://www.nichd.nih.gov/. 05/21/2013. Iliwekwa mnamo 3 March 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); External link in
(help)|website=
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 Kenyon, C; Colebunders, R; Crucitti, T (Desemba 2013). "The global epidemiology of bacterial vaginosis: a systematic review". American journal of obstetrics and gynecology. 209 (6): 505–23. PMID 23659989.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "What are the treatments for bacterial vaginosis (BV)?". http://www.nichd.nih.gov/. 07/15/2013. Iliwekwa mnamo 4 March 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); External link in
(help)|website=
- ↑ 6.0 6.1 6.2 "Bacterial Vaginosis (BV): Condition Information". http://www.nichd.nih.gov/. 05/21/2013. Iliwekwa mnamo 3 March 2015.
{{cite web}}
: Check date values in:|date=
(help); External link in
(help)|website=
- ↑ "Bacterial Vaginosis – CDC Fact Sheet". Centers for Disease Control and Prevention. Machi 11, 2014. Iliwekwa mnamo 2 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Mashburn, J (2006). "Etiology, diagnosis, and management of vaginitis". Journal of midwifery & women's health. 51 (6): 423–30. PMID 17081932.
- ↑ Othman, M; Neilson, JP; Alfirevic, Z (24 Januari 2007). "Probiotics for preventing preterm labour". The Cochrane database of systematic reviews (1): CD005941. PMID 17253567.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Bacterial Vaginosis (BV) Statistics Prevalence". cdc.gov. Septemba 14, 2010. Iliwekwa mnamo 3 Machi 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Viungo vya nje
hariri- Vaginosisi inayosababishwa na bakteria ni nini?
- Kuhusu Vaginosisi inayosababishwa na bakteria toka Center for Disease Control ya Marekani
- Makala kuhusu utafiti wa tiba mbadala za Vaginosis inayosababishwa na bakteria
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vaginosisi inayosababishwa na bakteria kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |