Vicente Bokalic Iglic
Vicente Bokalic Iglic C.M. (alizaliwa 11 Juni 1952) ni askofu wa Argentina wa Kanisa Katoliki. Aliongoza Jimbo la Santiago del Estero kama askofu kutoka 2013 hadi 2024, na baadaye akawa askofu mkuu wa kwanza wa jimbo hilo lilipoinuliwa hadhi kuwa jimbo kuu mnamo 22 Julai 2024. Wakati huohuo, alipewa cheo cha "Primate wa Argentina."
Bokalic aliteuliwa kuwa kardinali tarehe 7 Desemba 2024. Kabla ya uaskofu wake Santiago del Estero, alikuwa askofu msaidizi wa Buenos Aires kati ya 2010 na 2013, wakati ambapo askofu wake mkuu alikuwa Kardinali Jorge Bergoglio, ambaye baadaye alichaguliwa kuwa Papa Fransisko.[1]
Marejeo
hariri- ↑ "Mons. Bokalic, nuevo obispo de Santiago del Estero", Agencia Informativa Católica Argentina, 23 December 2013. (es)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |