Kichaka
(Elekezwa kutoka Vichaka)
Kichaka ni mmea wa kudumu wenye shina la ubao lakini, tofauti na mti, kina mashina zaidi ya moja. Tofauti nyingine ni urefu wake, ilhali vichaka kwa kawaida huwa na urefu wa sentimita kadhaa hadi mita 6 hivi.
Mimea mingi huweza kutokea ama kama kichaka au kama mti kutegemeana na mazingira yake. Kuna aina za miti mikubwa ambayo, ikikatwa, hukua tena kwa umbo la vichaka.
Vichaka mbalimbali ni muhimu kwa uchumi na kulimwa na binadamu kama vile mchai, mbuni na vichaka vingi vya matunda ya kuliwa.
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kichaka kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |