Vielezi vya mahali

Mifano
  • Leo nipo kazini hivyo hatuwezi kuonana
  • Babu yupo shambani


Vielezi vya mahali (alama yake ya kiisimu ni: E) ni maneno yanayofafanua kielezi kwa kujulisha mahali ambapo kitenzi hicho kinatendeka/kimetendeka.

Uchambuzi

hariri
Mifano
  • Mtoto amelala chumbani (mtoto = nomino ya kawaida, amelala = kitenzi kikuu, chumbani = kilezi cha mahali ambapo huyo mtoto amelala ni chumbani!)
  • Chui amepanda juu ya mti
  • Wanafunzi wamo darasani
  • Sote tutakwenda kuogelea baharini
  • Nyoka amejificha shimoni

Angalizo

hariri

Vielezi vya mahali hujengwa kwa kuambikwa (kuambikwa = kuambatanishwa) NI mwishoni mwa nomino inayokubali upatanisho wa kisarufi baada ya kuongezewa hiyo ni mwishoni mwake.

Mifano
Na. Nomino Kielezi
1 Shamba Shambani
2 Duka Dukani
3 Darasa Darasani
4 Mkono Mkononi
5 Choo Chooni
6 Sikio Sikioni
7 Kitanda Kitandani

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vielezi vya mahali kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.