Muazuki
(Vigna angularis)
Muazuki
Muazuki
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Nusufamilia: Faboideae (Mimea inayofanana na mharagwe)
Jenasi: Vigna
Savi
Spishi: V. angularis
(Willd.) Ohwi & H. Ohashi

Muazuki (Vigna angularis) ni mmea wa nusufamilia Faboideae katika familia Fabaceae. Mbegu zake huitwa azuki. Asili yake ni Asia ya Mashariki, Japani hasa. Katika Afrika ya Mashariki mmea huu hukuzwa mahali pachache, huko Somalia hasa. Azuki ni kiambato muhimu cha chakula cha Kisomali.