Mharagwe
(Phaseolus vulgaris)
Miharagwe inayopanda juu
Miharagwe inayopanda juu
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Planta (mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Fabales (Mimea kama mharagwe)
Familia: Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Jenasi: Phaseolus
L.
Spishi: P. vulgaris
L.

Mharagwe (pia: mharage) ni jina la mimea mbalimbali ya familia Fabaceae lakini mara nyingi sana Phaseolus vulgaris.

Mimea hii inatambaa au inapanda juu ya mimea mingine na matunda yake ni makaka marefu yaliyo na mbegu zinazoitwa maharagwe.

Licha ya mbegu hata makaka mabichi huliwa kama maharagwe-mboga.