Kinyunyizo

(Elekezwa kutoka Vinyunyizo)

Kinyuyizo ni chombo cha umwagiliaji mimea, ama kwenye shamba la kilimo au katika bustani. Matumizi mengine ni kwa ajili ya kupoza joto au kwa kupambana na vumbi nyingi. Majengo ya ofisi au viwanda mara nyingi huwa pia na mfumo wa vinyuyizo kwenye dari kwa kupambana na moto ikiwaka.

Kinyuyizo - mkono unaosukumwa na nguvu ya maji na kurudishwa kwa kamani unasababisha kichwa cha kuzunguka na kunwaga maji pande zote
Kinyunyizo kikubwa shambani kinachosogezwa polepole juu ya mazao kwa matairi

Kinyuyizo kinasambaza maji yanayofika mle kwa shinikizo kupitia mpira au bomba yakisukumwa kwa pampu. Njia nyingine kwa ajili ya maeneo madogo ni kutumia nguvu ya graviti kwa kutumia maji ya tangi iliyoko juu ya vinyuyizo.

Mara nyingi kichwa cha kinyuyizo huinuliwa juu kwa kusudi la kufikia eneo kubwa zaidi. Hasa katika bustani ya mapambo kuna muundo ambako mabomba ya kudumu yako chini ya ardhi na vinyukizo vinamwagilia sehemu za karibu tu.

Mfumo wa kisasa wa umwagiliaji wa matone unaweza kutumia vinyuyizo ingawa mara nyingi hutumia tu mabomba au mipira yenye matundu ambako maji yanahitajika.


Viungo vya Nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
 
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
  • Howser, Huell (Novemba 8, 2010). "Rainbird – California's Gold (12002)". California's Gold. Chapman University Huell Howser Archive.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)