Visiwa vya mfereji wa Kiingereza

Visiwa vya Mfereji wa Kiingereza ni funguvisiwa ya visiwa tisa katika Mfereji wa Kiingereza karibu na pwani la Ufaransa vyenye wakazi 160,000.

Visiwa vitano vikubwa ni:

Mahali pa Visiwa vya Mfereji wa Kiingereza

Kiutawala vimegawiwa kwa sehemu mbili: eneo la Jersey na eneo la Guernsey lakini visiwa kadhaa vina kiasi kikubwa cha uhuru pekee vyao.

Hali ya kisiasa hariri

Visiwa hivi vina hali ya pekee. Vyote ni "maeneo chini ya taji la Uingereza" lakini si sehemu za Ufalme wa Muungano au Uingereza mwenyewe. Havishiriki katika bunge la London wala havipaswi kupokea sheria za bunge hili bali vina bunge zao za Jersey, Guernsey, Alderney na Sark pamoja na watendaji na mahakama. Mfalme au malkia wa Uingereza ana wajibu wa kutetea visiwa na kushughulika mambo ya nje. Hali halisi wajibu hizi zinangaliwa na serikali ya Uingereza kwa niaba ya malkia.

Madaraka ya malkia (au: mfalme) yametokana na cheo chake cha kale kama Mtemi Mkuu wa Normandy miaka 800 iliyopita. Kihistoria visiwa vilikuwa sehemu ya Normandy na mwaka 1066 mtemi wa Normandy alishambulia na kuteka Uingereza. Kuanzia sasa wafuasi wake waliendelea na vyeo viwili vya Mfalme wa Uingereza na Mtemi wa Normandy na hivyo mkuu wa visiwa. Katika karne iliyofuata wafalme wa Ufaransa walitwaa Normandy lakini walishindwa kuteka viwia vidogo. Hali ya visiwa haikubadilishwa kisheria havikuunganishwa na ufalme wa Uingereza hivyo hadi leo ni mabaki madogo ya mali ya wafalme wa Uingereza katika Ufaransa wa leo.

Hivyo visiwa si sehemu za Uingereza wala sehemu za Umoja wa Ulaya viko ndani ya ushuru wa pamoja wa Ulaya lakini vina haki ya kuongeza kodi zao.

Mwakilishi wa malkia yaani serikali ya Uingereza ni Gavana.

Uchumi hariri

Uchumi wa visiwa umetegemea hasa utalii, huduma za benki na kilimo. Watu wengi huzungumza Kiingereza; hata hivyo wengine visiwani mwa Guernsey, Jersey na Sark huendelea kuongea lugha zao za asili.

Utamaduni hariri

Visiwa vyote vilikuwa na lugha zao ambazo ni aina za Kinormandy kinachozungumzwa pia kama lugha ya kieneo Ufaransa bara. Idadi ya wasemaji imepungua kuna hasa maelfu kadhaa Guernsey na Jersey. Lugha rtasmi kwa shughuli za serikali ni hasa Kiingereza lakini pia Kifaransa.

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Visiwa vya mfereji wa Kiingereza kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.