Vita ya Korea
Vita ya Korea ya karne ya 20 ilitokea kati ya mwaka 1950 na 1953.
Ilianzishwa na Korea ya Kaskazini iliyovamia Korea ya Kusini. Korea ya Kaskazini ilisaidiwa na Jamhuri ya Watu wa China na Umoja wa Kisovyeti. Korea ya Kusini ilisaidiwa na Marekani hasa. Lakini Marekani ilishiriki katika vita hii kwa jina la Umoja wa Mataifa pamoja na wanajeshi wa nchi 16.
Katika miaka mitatu ya vita hii mapigano ya maadui yalifika karibu kila sehemu ya rasi ya Korea na mateso ya wanachi raia pia ya wanajeshi kwenye pande zote yalikuwa mabaya sana. Si rahisi kutaja idada ya wahanga wote[1], lakini makadirio yanataja karibu milioni 4 watu raia na wanajeshi hadi milioni 1. [2]
Awamu nne za vita
haririShambulio la Kaskazini
haririKatika awamu ya kwanza kuanzia mwezi wa Mei 1950 jeshi la kaskazini lilivamia Korea ya Kusini likateka mji mkuu wa Seoul na kusukuma watetezi hadi kusini ya rasi ya Korea. Lililobaki mnamo Agosti/Septemba 1950 lilikuwa eneo la Pusan pekee.
Kuingilia kati kwa Umoja wa Mataifa na Marekani
hariri30 Julai 1950 Baraza la Usalama la UM iliamua kuingilia kijeshi dhidi ya uvamizi kutoka Korea Kaskazini. Azimio hii lilipita kwa sababu Umoja wa Kisovyeti hukuhudhuria kikao hivyo ulishindwa kupiga veto yake. Jeshi lililoingia kwa niaba ya Umoja wa Mataifa liliunganisha vikosi kutoka nchi 22, jumla askari 500,000 na wengi wao kutoka Marekani.
Katika awamu ya pili jeshi la Umoja wa Mataifa lilifika Pusan kuanzia Agosti 1950. Ndege za Marekani zilishambulia barabara, madaraja na jeshi la kaskazini kote kwenye rasi. Korea ya Kaskazini ilikosa ndege za kijeshi. Jeshi la Marekani na Korea Kusini lilelekea kaskazini kwa mbio na kuteka Seoul tena tar. 21 Septemba 1950. Likaendelea kuwarudisha Wakorea wa Kaskazini pia kuteka mji mkuu wa kaskazini Pyonyang tar. 19 Oktoba hadi kukaribia mpaka wa Korea na China kuanzia mwisho wa mwezi wa kumi 1950.
Hapa Wachina walitoa maonyo Wamarekani wasisongee mbele zaidi lakini jemadari mkuu MacArthur hakujali maonyo haya. Wachina waliandaa jeshi lao.
Kuingilia kwa China
haririKatika awamu ya tatu kuanzia Novemba 1950 jeshi la China likaingia kati na kuwasukuma Wamarekani kusini tena na kuteka Seoul mara ya pili tar. 3 Januari 1951. Ndege za kijeshi za Umoja wa Kisovyeti zilisaidia zikilinda anga nyuma ya mstari wa mapigano lakini bila kuwashambulia Wamarekani juu ya eneo lao. Wakati wa Januari Wachina waliweza kusogea mbele ndani ya Korea ya Kusini lakini walikwama kwa sababu walishindwa kupata mahitaji yao kutokana na nguvu ya Marekani angani.
Kurudi kwa hali ya awali
haririKatika awamu ya mwisho hadi Julai 1951 mashambulio ya Kaskazini na Kusini yalibadilishana na Wachina walirudishwa polepole hadi mpaka wa 38 °C latitudo uliowahi kuwa mpaka kabla ya vita. Marekani iliamua kutosogea mbele zaidi ikitafuta majadiliano ya kusimamisha vita.
Majadiliano haya yalianza 10 Julai 1951 yakaendelea hadi 1953. Muda wote vita iliendelea kwa njia ya mashambulizi kila upande lakini kwa shabaha ya kushika maeneo yaliyowahi kuwa upande mmoja au mwingine kabla ya vita lakini kushikwa na adui kwa sasa.
Tar. 27 Julai 1953 mapatano ya kusimamisha vita yalifikiwa. Eneo lenye upana wa kilomita nne pande zote mbili za mstari wa latitudo ya 38 lilitangazwa kuwa "Ukanda usio na jeshi".
Hadi leo ni mpaka kati ya nchi zote mbili za Korea na kulindwa na wanajeshi wengi sana.
Marejeo
hariri- ↑ Sehemu ya watu raia waliuawa ovyo na jinai hizi hazikutolewa taarifa kamili; kila upande ulijaribu kupanusha iadi ya wafu wa wanajeshi wa upande mwingine na kupunguza idadi ya wafu wao wenyewe
- ↑ linganisha hitimisho ya Xu Yan Korean War: In the View of Cost-effectiveness tovuti ya Konsuli kuu ya Jamhuri ya China New York, iliangaliwa Aprili 2017
Viungo vya Nje
haririKihistoria
hariri- Anniversary of the Korean War Armistice: Truman on Acheson's Crucial Role in Going to War Ilihifadhiwa 21 Februari 2015 kwenye Wayback Machine. Shapell Manuscript Foundation
- Korean War resources, Dwight D. Eisenhower Presidential Library Ilihifadhiwa 26 Juni 2014 kwenye Wayback Machine.
- North Korea International Documentation Project
- Grand Valley State University Veteran's History Project digital collection Ilihifadhiwa 21 Aprili 2012 kwenye Wayback Machine.
- The Forgotten War, Remembered – four testimonials in The New York Times
- Collection of Books and Research Materials on the Korean War Ilihifadhiwa 27 Aprili 2021 kwenye Wayback Machine. an online collection of the United States Army Center of Military History
- Korean War, US Army Signal Corps Photograph Collection Ilihifadhiwa 5 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine. US Army Heritage and Education Center, Carlisle, Pennsylvania
- The Korean War at History.com
- Korean-War.com
- Koreanwar-educator.org
Media
hariri- The Korean War You Never Knew – slideshows by Life magazine
- QuickTime sequence of 27 maps adapted from the West Point Atlas of American Wars
- Animation for operations in 1950
- Animation for operations in 1951
- US Army Korea Media Center official Korean War online image archive
- Rare pictures of the Korean War from the U.S. Library of Congress and National Archives
- The Korean War in Color katika YouTube
- Land of the Morning Calm Canadians in Korea – multimedia project including veteran interviews Ilihifadhiwa 10 Septemba 2013 kwenye Wayback Machine.
- Pathé Ilihifadhiwa 6 Januari 2012 kwenye Wayback Machine. Filamu za jeshi la Kiingereza kutoka vita ya Korea
- CBC Digital Archives—Forgotten Heroes: Canada and the Korean War
- crime of Korea, filamu ya propaganda ya arekani mnamo 1950