Korea Kusini

(Elekezwa kutoka Korea ya Kusini)

Korea ya Kusini (jina rasmi: Jamhuri ya Korea) ni nchi ya Asia ya Mashariki iliyopo kusini mwa rasi ya Korea.

대한민국 Daehan Minguk
Jamhuri ya Korea
Bendera ya Korea ya Kusini Nembo ya Korea ya Kusini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: 널리 인간을 이롭게 하라 "Lete faida kwa watu wote"
Wimbo wa taifa: Aegukga
(Wimbo la Taifa)
Lokeshen ya Korea ya Kusini
Mji mkuu Seoul
37°35′ N 127°0′ E
Mji mkubwa nchini Seoul
Lugha rasmi Kikorea
Serikali Jamhuri
Moon Jae-in (문재인 , 文在寅)
Kim Boo-kyum (김부겸 , 金富謙)
Kuundwa kwa
Ufalme wa Gojoseon
Tangazo la uhuru bado chini ya Japani
Ukombozi kutoka utawala wa Japani
Jamhuri ya kwanza
ilitambuliwa na Umoja wa Mataifa

3 Oktoba 2333 KKa
1 Machi 1919
15 Agosti 1945
15 Agosti1948
12 Desemba 1948
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
100,210 km² (ya 108)
0.3
Idadi ya watu
 - Julay 2014 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
50,617,045 (ya 26)
505.1/km² (ya 13)
Fedha Won ya Korea Kusini (KRW)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
Wakati sanifu wa Korea (UTC+9)
-- (UTC+9)
Intaneti TLD .kr
Kodi ya simu +82

-


Ramani ya Korea ya Kusini

Upande wa kaskazini imepakana na Korea ya Kaskazini. Korea zote mbili zilikuwa nchi moja hadi mwaka 1945 chini ya utawala wa kikoloni wa Japani.

Ng'ambo ya bahari iko Uchina upande wa magharibi na Japani upande wa kusini-mashariki.

Mji mkuu, pia mji mkubwa, ni Seoul ambako karibu nusu ya wakazi wote huishi ama mjini ama katika mazingira yake. Seoul ni kati ya miji muhimu ya biashara na uchumi kimataifa.

Historia

hariri

Utamaduni wa Korea ni kati ya zile za kale zaidi duniani.

Tangu maungano ya kitaifa ya Korea yote mwaka 668 KK ilikuwa nchi moja hadi mwaka 1910 ilipofanywa koloni la Japani.

Uhuru baada ya mwaka 1945 ulifuatwa na mgawanyiko wa nchi na kuundwa kwa Korea Kusini.

Awali ilikuwa nchi maskini yenye uchumi wa kilimo, lakini iliendelea kuwa nchi ya viwanda iliyofaulu kusogea mbele na kujenga demokrasia imara.

Siku hizi imekuwa moja ya nchi tajiri ya Asiaː ina nafasi ya 13 duniani kati ya mataifa matajiri. Iko kati ya nchi kumi duniani zinazouza bidhaa nyingi nje.

Hali ya maisha ni ya juu na viwanda vyake vinatengeneza bidhaa za kisasa kabisa kama motokaa, meli, mashine, vifaa vya kompyuta na nyinginezo.

Kuna mikoa tisa nchini Korea Kusini, zikiwemo:

Wakazi karibu wote (99 %) ni Wakorea asili. Wachina ni 1.8 %, lakini wengi wao wana asili ya Korea.

Idadi ya watu inaelekea kupungua kutokana na uzazi kuwa wa nadra mno (watoto 9 kwa watu 1,000ǃ).

Lugha rasmi na ya kawaida ni Kikorea.

Kiasili watu wa Korea walifuata dini ya jadi iliyoheshimu mapepo mbalimbali na kutoa sadaka kama njia za kuyapatanisha.

Tangu karne ya 4 Ubuddha uliingia kutoka China ukawa dini rasmi.

Ukonfusio ulifuata tangu karne ya 13.

Ukristo ulingia pia kutoka China ukaanza kukua zaidi tangu karne ya 19.

Siku hizi takriban nusu ya Wakorea wa kusini wasema hawana dini. Sehemu kubwa wanakadiriwa kuwa wafuasi wa Konfusio lakini hawajiiti "wanadini".

Ukristo ni kundi kubwa la kidini ukiwa na 29 % za Wakorea wa Kusini, wakiwemo Waprotestanti (18.3 %) na Wakatoliki (10.9 %). Wabuddha ni kama 22.8 %. Kuna pia wafuasi wachache wa dini nyingine mbalimbali.

Tazama pia

hariri

Viungo vya nje

hariri
 
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Uajemi | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.