Vitamini C

(Elekezwa kutoka Vitamin C)

Vitamini C ni vitamini inayopatikana hasa katika matunda na majani mabichi. Kikemia ni aina ya asidi askobini na binadamu ni kati ya spishi chache ambazo haziwezi kutengeneza asidi hii mwilini. Kwa hiyi watu hutegemea chakula chenye kiwango cha vitamini hii.

ascorbic acid
Viazi katika ganda huwa na 20 mg/100 g za vitamini C

Vitamini C ina kazi muhimu katika mchakato wa kupona vidonda mwilini. Uhaba wake kwa muda mrefu unasababisha ugonjwa wa kiseyeseye (au hijabu). Kiseyeseye husababisha ufizi wa meno kuwa na vidonda na pia vidonda vingine mwilini kutopoa. Ugonjwa huu ulijulikana hasa wakati wa safari ndefu za baharini. Zamani haikujulikana chanzo chake kilikuwa nini; meli na jahazi zilibeba tu unga wa mkate au mchele kama chakula kilichoongezwa kwa nyama kavu au samaki kutoka baharini lakini matunda hayakuwa kawaida. Mabaharia wengi waligonjeka na kufa. Katika karne ya 19 mabaharia walitambua ya kwamba akiba ndogo ya malimau inaweza kuokoa watu kama wanakunjwa kijiko cha maji ya limau kila baada ya siku kadhaa.

Mwaka 1928 vitamini C iligundiuliwa pia kikemia na tangu 1928 ilithibitishwa kuwa inasmimamisha kiseyeseye.

Mahitaji ya mwili hukadiriwa kuwa miligramu 60-100 kwa siku; kiwango hiki kinapatikana kwa njia ya chakula cha kawaida.

Vyanzo

hariri

Matunda kama limau, chungwa na balungi ni vyanzo bora vya vitamini C. Kwa jumla karibu matunda yote yenye ladha ya kichungu ni chanzo chake.

Kuna pia aina za nyama na samaki zinazopeleka vitamini C mwilini. Hapo ndipo sababu ya kwamba Waeskimo hawakuwa na kiseyeseye ingawa zamani waliishi bila matunda kwa miezi mingi lakini walikula samaki bichi.

Kupika chakula kwa muda mrefu kunaharibu asidi ya vitamini C.


Jedwali inayoonyesha kiwango cha Vitamini C katika matunda na mboga
Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda Matunda mg vitamini C kwa kila gramu 100 za tunda
CamuCamu 2800 Limau 40 Mizabibu 10
Rose hip 2000 Melon, cantaloupe 40 Apricot 10
Acerola 1600 Cauliflower 40 Plum 10
Jujube 500 Grapefruit 30 Watermelon 10
Baobab 400 Raspberry 30 Ndizi 9
Blackcurrant 200 Tangerine/ Mandarin oranges 30 Karoti 9
Indian gooseberry 445 Passion fruit 30 Avocado 8
Guava 100
Kiwifruit 90 Spinach 30 Crabapple 8
Broccoli 90 Cabbage Raw green 30 Peach 7
Loganberry 80 Lime 20 Tofah 6
Redcurrant 80 Mango 20 Blackberry 6
Brussels sprouts 80 Melon, honeydew 20 Beetroot 5
Lychee 70 Raspberry 20 Pear 4
Persimmon 60 nyanya 10 Lettuce 4
Papaya 60 Blueberry 10 Cucumber 3
Strawberry 50 mananasi 10 Fig 2
Orange 50 Pawpaw 10 Bilberry 1
+ Jedwali inayoonyesha kiwango cha Vitamini C katika nyama na samaki
Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula Aina ya nyama mg vitamini C kwa gramu 1000 za chakula
Ndama maini (bichi) 36 Kuku maini (fried ) 13 Mbuzi maziwa (bichi) 2
ng’ombe maini (bichi) 31 Kondoo maini (ya kuchoma) 12 NYama ya ng’ombe nyekundu (ya kuchoma) 0
Oysters (bichi) 30 Lamb heart (ya kuchoma) 11 Mayai ya kuku (bichi ) 0
Cod Roe (ya kuchoma) 26 Kondoo ulimi (stewed) 6 Nyguruwe Bacon (ya kuchoma) 0
Nguruwe maini (bichi) 23 Maziwa ya binadamu (bichi) 4 Nyama ya ndama (ya kuchoma) 0
Lamb brain (ya kupikwa) 17 Cows maziwa (bichi) 2 Chicken leg (ya kuchoma) 0


Marejeo

hariri