Viunganishi
Mifano |
---|
|
Viunganishi ni neno au kikundi cha maneno chenye kuunganisha vipashio vya lugha ili kuunda kipashio kikubwa zaidi. Pia ni maneno yanayounganisha maneno mengine. Kiunganishi kinaweza kuunganisha neno na neno, kirai na kirai, kishazi na kishazi, sentensi na sentensi au vinginevyo.
Uchambuzi
hariri- Mifano ya jumla
- Baba na mama
- Analima bila kupanda
- Baba analima na baba anapanda
- Shoka limeshindwa sembuse panga
Maumbo ya viunganishi
haririViunganishi havina maneno ya kupambikwa katika neno au katika kupatanishwa kisarufi ndani ya tungo. Yaani, mfano cheza, chezewa, chezeka, na kadhalika. Hayo ni maumbo ya maneno ambayo hayabadiliki.
- Mfano
Na, lakini, ingawa, bila, au, ila, sembuse, kwa sababu, kwa kuwa, pamoja na, ijapokuwa, tena, iwapo, labda, toka, n.k.
Aina za viunganishi
haririKuna aina mbili za viunganishi - navyo ni:
Ama:
Viunganishi huru ni vile vinavyosimama pekee katika tungo/katikati ya vipashio vinavyoungwa. Kwa mfano: Sisi tunaimba na kucheza.
Viunganishi tegemezi ni vile ambavyo huunda kwa viambishi vya o-rejeshi vinavyowekwa katika kishazi huru kwa pamoja huunda sentensi changamano. Viambishi hivyo ni kama vile: po, ye, lo, cho n.k. Kwa mfano: Mama anayepika ni msusi.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Viunganishi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |